EWURA NA MAMLAKA YA PETROLI UGANDA WARIDHISHWA NA MAENDELEO UJENZI MIUNDOMBINU MRADI BOMBA LA MAFUTAZiara katika kiwanda cha kupasha mafuta joto mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga.

Na Marco Maduhu, NZEGA.

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Mamlaka ya Petroli Uganda (PAU), wametembelea kuona maendeleo ya ujenzi wa
  Kiwanda cha miundombinu ya bomba la mafuta(Coating Plant) kilichopo kijiji cha Sojo Kata ya Igusule wilayani Nzega katika mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda kwenda Bandari ya Tanga.

Mkurugenzi wa Petroli kutoka EWURA Gerald Maganga akizungumza jana wakati wa ziara hiyo ya ukaguzi wa ujenzi wa miundombinu kiwanda hicho, amesema wameambatana na wajumbe wa Bodi na Menejimenti kutoka Mamlaka ya Petroli Uganda na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, ili kuona maendeleo ya ujenzi miundombinu wa mradi wa bomba la mafuta ghafi.

Amesema katika ziara hiyo wameanzia Tanga kuona maendeleo ya ujenzi wa Matanki ya kuhifadhia mafuta, wakapita Singida hadi kwenye kiwanda hicho cha kupasha mafuta joto kilichopo kijiji cha Sojo wilayani Nzega, ambacho ameeleza kuridhishwa na hatua ya ujenzi ulipofikia hivi sasa.

“Tupo katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya mradi wa bomba la mafuta ghafi, ambalo linatoka Hoima nchini Uganda hadi Chogoleani Tanga, na katika kiwanda hiki cha kupasha mafuta joto tumeona maendeleo makubwa ya ujenzi na kazi inakwenda vizuri,”amesema Maganga.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Petroli Uganda (PAU) Ernest Rubondo, amepongeza hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa miundombinu katika mradi huo wa bomba la mafuta ghafi nchini Tanzania, huku akisisitiza vijana wa maeneo husika ambao wanapitiwa na mradi huo wapewe kipaumbele cha ajira.

“Ziara yetu hapa Tanzania ni kuona maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya bomba la mafuta ghafi, tumeanzia Tanga tukaja Singida na sasa tupo hapa kijiji cha Sojo wilayani Nzega na tutapita pia Kagera, hatua ya ujenzi iliyofikiwa ni nzuri tumefurahi sana,”amesema Rubondo.

Balozi wa Uganda nchini Tanzania Kanali Fred Mwesiggye, amesema mradi huo wa bomba la mafuta ghafi, umeendelea kuimarisha mahusiano mazuri baina ya nchi hizo mbili Tanzania na Uganda, na wananchi wake watanufaika kwa kupata kazi na kuinuka kiuchumi pamoja na mataifa yao kwa ujumla.

Kaimu Meneja wa Kiwanda  cha miundombinu ya bomba la mafuta Coating Plant) kilichopo kijiji cha Sojo Kata ya Igusule wilayani Nzega Wiliam Kajagi, amesema ujenzi wa kiwanda hicho unaendelea vizuri na sasa upo asilimia 43, huku akibainisha kuwa wamezingatia pia suala la kuajiri wazawa na asilimia 80 ya vijana walioajiriwa wanatoka wilayani Nzega.

Balozi wa Uganda nchini Tanzania Kanali Fred Mwesiggye akizungumza kwenye ziara hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Petroli Uganda (PAU) Ernest Rubondo akizungumza kwenye ziara hiyo.

Mkurugenzi wa Petroli kutoka EWURA Gerald Maganga,akizungumza kwenye ziara hiyo.

Kaimu Meneja wa Kiwanda cha kupasha mafuta joto kilichopo kijiji cha Sojo Kata ya Igusule wilayani Nzega Wiliam Kajagi, akielezea hatua za ujenzi wa kiwanda hicho ulipofikia kuwa ni asilimia 43.

Ziara ya kuona maendeleo ya ujenzi wa kiwanda wa kiwanda cha miundombinu ya bomba la mafuta ghafi ikiendelea.

Ziara ya kuona maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha miundombinu ya mradi wa bomba la mafuta ghafi ikiendelea.

Ziara ya kuona maendeleo ya ujenzi wa kiwanda miundombinu ya mradi wa bomba la mafuta ghafi ikiendelea.

Kaimu Meneja wa Kiwanda cha miundombinu ya bomba la mafuta katika kijiji cha Sojo Kata ya Igusule wilayani Nzega Wiliam Kajagi, (kulia) akionyesha Mchoro wa Ramani ya ujenzi wa kiwanda hicho.

Kaimu Meneja wa Kiwanda cha miundombinu ya bomba la mafuta katika kijiji cha Sojo Kata ya Igusule wilayani Nzega Wiliam Kajagi, (kulia) akionyesha Mchoro wa Ramani ya ujenzi wa kiwanda hicho.

Kaimu Meneja wa Kiwanda cha miundombinu ya bomba Mafuta (Coating Plant) kilichopo kijiji cha Sojo Kata ya Igusule wilayani Nzega Wiliam Kajagi, akitoa maelezo juu ya ujenzi wa kiwanda hicho.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Petroli Uganda, (kushoto) Ernest Rubondo, akiuliza swali katika ujenzi wa Kiwanda cha miundombinu ya mradi wa bomba la mafuta ghafi.

Muonekano maendeleo ya ujenzi wa kiwanda.

Awali Balozi wa Uganda nchini Tanzania Fred Mwesiggye (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Petroli kutoka EWURA Gerald Maganga wakisikiliza maelezo ya ujenzi wa Kiwanda cha miundombinu ya mradi wa bomba la mafuta ghafi.

Balozi wa Uganda nchini Tanzania Fred Mwesiggye, (kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Petroli Uganda Ernest Rubondo wakisikiliza maelezo ya ujenzi wa Kiwanda, cha miundombinu ya mradi wa bomba la mafuta ghafi.

Mkurugenzi wa Petroli EWURA Gerald Maganga (kulia) akiangalia Mchoro wa Ramani ujenzi wa Kiwanda cha Miundombinu ya mradi wa bomba la mafuta ghafi.

Wajumbe wa Bodi na Menejimenti kutoka Mamlaka ya Petroli Uganda wakisiliza maelezo ya ujenzi wa Kiwanda cha miundombinu ya mradi wa bomba la mafuta ghafi ambalo linatoka Hoima Uganda hadi Tanga.

Usikilizaji maelezo ujenzi wa Kiwanda cha miundombinu ya , Mradi wa bomba la mafuta ghafi ukiendelea.

Picha ya pamoja ikipigwa katika ujenzi wa Kiwanda cha  miundombinu ya mradi wa ujenzi bomba la mafuta ghafi katika kijiji cha Sojo wilayani Nzega.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post