MKE, MME MBARONI TUHUMA ZA KUMUUA MAMA MZAZI USHIRIKINA GEITAWatu wawili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Geita kwa tuhuma ya kumuua kwa kumchinja Mwanamke Mmoja aliyetambulika kwa jina la Butamo Igonzele (70) Mkazi wa kijiji cha Bumegezi Kata ya Ihanamilo wilaya ya Geita Mkoani Geita.

Akizungumza na Wandishi wa Habari Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Kamishna Msaidizi wa Polisi Berthaneema Mlayi amesema watu hao wanashikiliwa na Jeshi hilo kwa ajili ya upelelezi wa kina ili kubaini wahusika.

Amesema watuhumiwa hao wamemakatwa baada ya uchunguzi wa awali kuonyesha wanaweza kuhusika katika mauaji hayo huku jitihada zikifanyika katika kujiridhisha kupitia uchunguzi wa awali.

Kaimu Kamanda amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Joyce Julius ambaye ni Mtoto wake na Marehemu na Juma Charles ambaye ni Mkwe wa Marehemu ambao inadaiwa walikuwa wanamtuhumu Marehemu kuhusika na kifo cha mtoto wao ambaye alifariki wiki Moja iliyopita

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments