VIONGOZI WA KAMATI YA UTEKELEZAJI JUMUIYA YA WAZAZI CCM DAR ES SALAAM WAPEWA SEMINA


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Abbas Mtemvu akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Viongozi wa Kamati ya utekekezaji yaliyoanza leo katika hotel ya Star Breeze Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Abbas Mtemvu akifungua mafunzo ya siku tatu ya Viongozi wa Kamati ya utekekezaji yaliyoanza leo katika hotel ya Star Breeze Kigamboni, jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Abbas Mtemvu akisisitiza jambo wakati akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Viongozi wa Kamati ya utekekezaji yaliyoanza leo katika hotel ya Star Breeze Kigamboni, jijini Dar es Salaam.Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Abbas Mtemvu akiwasili na kupokelea na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salam, Bi.Khadija Ally katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Viongozi wa Kamati ya utekekezaji yaliyoanza leo katika hotel ya Star Breeze Kigamboni, jijini Dar es Salaam. Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bw.Adam Ngallawa akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Viongozi wa Kamati ya utekekezaji yaliyoanza leo katika hotel ya Star Breeze Kigamboni, jijini Dar es Salaam.Katibu wa Organization ya Wazazi CCM Taifa Bw.Saidi King'eng'ena akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Viongozi wa Kamati ya utekekezaji yaliyoanza leo katika hotel ya Star Breeze Kigamboni, jijini Dar es Salaam.Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salam, Bi.Khadija Ally akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Viongozi wa Kamati ya utekekezaji yaliyoanza leo katika hotel ya Star Breeze Kigamboni, jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Abbas Mtemvu akipata picha ya pamoja na Viongozi wa kamati ya Utekelezaji katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Viongozi hao yaliyoanza leo katika hotel ya Star Breeze Kigamboni, jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Abbas Mtemvu akipata picha ya pamoja na watoa Mafunzo katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Viongozi wa Kamati ya utekekezaji yaliyoanza leo katika hotel ya Star Breeze Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

***********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Uongozi wa Kamati ya Utekelezaji wametakiwa kuendeleza mshikamano na ushirikiano ili kuhakikisha kazi zinatendeka kupitia Ilani ya CCM ili wanachama na wananchi kwa ujumla waendelee kuwa na imani na Chama hicho.

Ameyasema hayo leo Januari 12,2023 Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Abbas Mtemvu wakati akifungua Semina ya Siku tatu ya Uongozi wa Kamati ya Utekelezaji iliyoandaliwa na Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam.

Amesema kuna umuhimu wa viongozi wa chama hicho kuhakikisha kamati ya Siasa kutoa hamasa kwa wanachama na wananchi kwa ujumla ili kuhakikisha Chama hicho kinafanya vizuri katika chaguzi zijazo.

Aidha amewataka viongozi hao kushuka kwenye kata, wilaya na matawi kutoa elimu kuhusu masuala ya chama hasa Ilani ya Chama na utekelezaji wake katika maeneo mbalimbali kwenye mkoa wa Dar es Salaam.

Amesema kuna changamoto ya upatikanaji wa kadi za uanachama ingawa wanachama wengi wanaingia kwenye chama hicho hivyo ameshalifikisha kwenye uongozi wa juu na linashughulikiwa ikiwezekana uwepo wa mfumo wa kielektroniki.

"Wanachama wengi sasa wanahitaji kuja CCM lakini upatikanaji wa kadi zetu ni tatizo kwahiyo nitaliwasilisha kwa kinamna yake kwa mwenyekiti suala hili la kadi walipe kipaumbele ikiwezekana ziweze kupatikana kwa wakati". Amesema

Kwa upande wake Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bw.Adam Ngallawa amewasihi kamati ya utekelezaji wa chama cha Mapinduzi kuhakikisha wanatumia michango kutekeleza miradi mbalimbali ili Juhudi za Jumuiya ya Wazazi zionekane na wanachama kuwa na imani na Chama hicho.

Amewataka viongozi wa kamati ya Utekelezaji kuwa kiungo kwa wazazi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam na kwa wananchi wa mkoa huo kwani ndani yenu wamo vijana, wanawake,hivyo wametakiwa kuhakikisha Chama kinakuwa imara.

Nae Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salam, Bi.Khadija Ally amesema watahakikisha wanahamasiisha ili ushindi wa kishindo unapatikana katika mkoa wa Dar es Salaam kwani wamejipanga kikamilifu kufanya vizuri kwenye kuelekea chaguzi zijazo.

Amesema kwa kuwa amechaguliwa kwa kuaminiwa hatahikikisha anatoa ushirikiano wa kutosha katika utekelezaji wa chama hicho na ndo maana wakaona kuna umuhimu wa kupata mafunzo ya uongozi ili kila mmoja ajue mipaka yake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post