KIATU KINAVYOTAMBULISHA HADHI YA MWANAUME MTANASHATINa Dotto Kwilasa.

Kila mwanaume anahitaji kuwa na mwonekano wa kipekee machoni pa watu bila kujali ni wakati gani au mahali gani..na hii ni kwa wanaume wa kisasa,wanaoenda na wakati .

Mwonekano wa mwanaume huanzia pale chini kabisa kwenye miguu upande wa viatu ,haijalishi ukubwa wa bei ya kiatu husika kinachotazamwa zaidi ni ubora na dizaini ya kiatu na mapenzi ya mtumiaji mwenyewe.

Wanawake wengi wamekuwa wakivutiwa na wanaume wenye hadhi fulani ivi ya kisasa kwa kuzingatia mtazamo wa uvaaji wa viatu vizuri,vyenye hadhi na muonekano wa kuvutia.

Ngoja nikuibie Siri,kuna siku nikiwa kwenye harakati zangu za maisha nilikutana na wadada wakizungumza kuhusu muonekano mzima wa mwanaume kuwa mara nyingi wao huvutiwa zaidi na kiatu .

Yani mwanamke anapokutana na mwanaume njiani kitu cha kwanza anachozingatia kabla ya mambo mengine ni kiatu,anaangalia kiatu kina hadhi??…kama mwanaume hajijali hata akiwa na mwanamke wake hawezi kumjali..

Wanawake wanazingatia zaidi upekee wa mwanaume kuanzia viatu kabla ya muonekano mwingine kama mavazi,pafyumu namna anavyonyoa,anavyo zungumza na mwendo wake..

Kwa kifupi tu sio kila kiatu ni kiatu,mwanaume unapaswa kuzingatia katika utaratibu wako wa mitoko hukosi viatu vya matukio tofauti tofauti mfano kwenye sherehe,mitoko ya kawaida, kazini na safarini,namaanisha kiatu unachovaa kiendane na unachoenda kukifanya kwa wakati huo.


Cha kuzingatia zaidi unapaswa kwenda na wakati bila kujali nafsi yako inapenda Nini..kikubwa hapa ni kwenda na wakati na kuwa na mvuto wa kidigitali . 
Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

Post a Comment

Previous Post Next Post