BUNGE LAANZISHA UTARATIBU WA BONANZA LA MICHEZO

 


Na Dotto Kwilasa, DODOMA.


SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Tulia Ackson amesema Bunge hilo limeanzisha utaratibu wa kuwa na Bonanza la michezo mara nne kwa mwaka kwa Wabunge na Watumishi wa Bunge .


Amesema bonanza hilo  limegawanywa Katika makundi ambapo kutakuwa na mabonanza madogo matatu wakati wa mikutano mifupi  ya Bunge na bonanza moja kubwa wakati wa mkutano wa Bajeti.

 

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Bungeni Jijini hapa Spika huyo wa Bunge amesema  bonanza hilo litahusisha michezo mbalimbali ambayo ni pamoja na mpira wa miguu,mpira wa wavu,Pool table,kurusha vishale,riadha,karata,pamoja na bao.

 

Ametaja michezo mingine kuwa ni pamoja na Draft,mpira wa meza,kukimbia na kijiko,kukimbia na chupa,kukimbia na glass ikiwa na maji pamoja na kushindana kunywa soda na chakula kwa haraka.

 

"Lengo la mabonanza hayo ni kutoa fursa ya kuwakutanisha Wabunge,Watumishi wa Ofisi ya Bunge pamoja na wadau mbalimbali katika mazingira rafiki nje ya ofisi  na hivyo kuleta kufahamiana zaidi na kujenga umoja utakaosaidia katika utekelezaji wa majukumu yao,"amesema.

 

Dk.Tulia pia amesema kuwa," kuanzishwa kwa Bunge Bonanza hakufuti ushiriki wetu katika michezo mingine ya kirafiki na michezo inayotukutanisha na wanamichezo wengine kutoka Mabunge mengine ikiwa ni pamoja na michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki(EALA),"amesema 

 


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

Post a Comment

Previous Post Next Post