RIDHIWANI KIKWETE AHAMASISHA UPANDAJI MITI SHULENI




Naibu Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mh. Ridhiwani Kikwete akipanda mti ikiwa ishara ya kuunga mkono jitihada za uhifadhi wa mazingira.



NA. ELISANTE KINDULU, CHALINZE

NAIBU Waziri wa ardhi ,nyumba na naendeleo ya makazi Mh. Ridhiwani Kikwete amezihamasisha shule za Msingi na Sekondari kupanda miti ili kusaidia kutunza mazingira.

Mh. Ridhiwani aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na walimu, wanafunzi na watendaji wa Serikali wa Mji wa Chalinze katika viwanja vya shule ya Msingi Bwilingu "A" mjini hapa hivi karibuni.

Mh. Ridhiwani ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Chalinze aliishukuru menejimenti ya DSTV kwa kushirikiana na UN global compact kwa kuendesha mpango mahususi wa kampeni dhidi ya uhifadhi wa mazingira hususani kampeni dhidi ya upandaji miti.

Naibu Waziri huyo wa ardhi alisema taasisi na  wananchi wanapaswa kupanda miti kwa wingi ili kuweza kuhifadhi mazingira ikiwamo na kuondokana na hewa ya ukaa ambayo inaathari kubwa kwa maisha ya binadamu na viumbe hai kwa ujumla.

Mh. Ridhiwani alipata pia fursa ya kupanda mti ikiwa ishara ya kuunga mkono juhudi za DSTV na washirika wake wa UN global compact katika uhifadhi wa mazingira.

Naibu Waziri Ridhiwani akihitimisha hafla hiyo aliwagawia wawakilishi wa shule 10 za Msingi  na Sekondari miti ya matunda na kivuli ambapo Kila  shule ilinufaika na miti 200 baada ya wahisani hao wa DStv na UN global compact kutoa jumla ya miti  2000 kwa kuanzia katika baadhi ya shule katika halmashauri ya Chalinze mkoa wa Pwani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments