MZEE WA MIAKA 71 AFARIKI AKILA MAISHA NA MREMBO GESTIPolisi wanachunguza kisa ambapo mwanamume mmoja wa miaka 71 ambaye ameaga dunia kwenye lojingi akiwa na binti wa umri wa miaka 22 mtaani Parklands, jijini Nairobi.

Mwanamke huyo aliambia polisi kuwa walikodi chumba kwenye lojingi hiyo na muda mfupi baadaye mwanamume huyo alianza kuhema akitaka hewa.

Alianza kulalamikia maumivu ya kifua na mgongo kabla ya mikono na miguu yake kufa ganzi.

Mwanamke huyo alikimbia nje ya jengo kutoka ghorofa ya tatu na kuomba dereva wa taxi aliyekuwa kwenye lango kumsaidia kuokoa uhai.

Dereva huyo alitumia gari la mwendazake kumpeleka katika hospali ya karibu - Aga Khan - ambako alisemekana kuwa ameaga dunia.

Maafisa wa polisi waliitwa eneo la tukio na kunakili kisa hicho kabla ya mwili kupelekwa katika makafani.

Polisi walibaini kuwa wawili hao walienda kwenye chumba hicho Alhamisi mwendo wa saa kumi alasiri na mwendazake alianza kulalamika kuhusu maumivu saa mbili baadaye.

Polisi wanasema kuwa wanachunguza kisa hicho. Visa hivyo vimekithiri katika lojingi za jijini na vingi ripoti za upasuaji zinasema kuwa vinatokana na mshutuko wa moyo, polisi wamesema.

Via: Tuko News

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

Post a Comment

Previous Post Next Post