MWALIMU AKUTWA AMEFARIKI KWENYE GHETO LA MPENZI WAKE

Polisi wanasaka jamaa ambaye mpenziwe aliyekuwwa anasomea ualimu amepatikana akiwa amefariki dunia katika nyumba yake mjini Nakuru nchini Kenya.

Mwili wa msichana huyo mwenye miaka 19 ulipatwa nyumbani kwa jamaa huyo katika mtaa wa Naka baada ya uvundo kuwapiga wakazi.

Ripoti zinasema msichana huyo alikuwa ni mwanafunzi wa chuo cha Karatina ambapo alikuwa akisomea kuwa mwalimu wa Hisabati na Biolojia. Mwili wa Phyllis Jepleting ulipatikana katika kitanda ukiwa umeangalia kichwa chini huku ukivuja damu.

Majirani wanasema mwenye nyumba hajakuwepo kwa siku kadhaa na ndipo wakaita polisi baada ya kupata uvundo. 

Msichana huyo alikuwa katika mwaka wake wa kwanza chuo hicho na ni kutoka eneo bunge la Aldai kaunti ya Nandi kwa mujibu wa stakabdhi zilizopatikana. 

Mwili wake umepelekwa katika kituo cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya kaunti ya Nakuru maarufu kama PGH.

Jamaa mwenye nyumba hiyo anaripotiwa kuzima simu tangu sikuu ya Disemba 26 na hajulikani alipo.

Chanzo - Tuko news

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post