WAANDISHI WA HABARI LINDI WAHIMIZWA KUTHAMINI KAZI NA TAALUMA YAO

Waandishi wa habari mkoani Lindi wamehimizwa wathamini kazi na taaluma yao ya uandishi wa habari ili taaluma hiyo na wao wenyewe waweze kuthaminiwa.

Wito huo ulitolewa juzi na mkuregenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kilwa, Eston Ngilangwa wakati wa mkuu mkutano mkuu maalumu wa klabu ya waandishi wa habari wa mkoa wa Lindi (Lindi Regional Press Club) uliofanyika katika manispaa ya Lindi.

Ngilangwa ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mkutano huo, alisema ili taaluma ya uandishi wa habari na waandishi wa habari wenyewe waweze kuthaminiwa hawana budi kuthamini taaluma hiyo kwa kulinda miiko na sheria, ikiwemo kuzingatia maadili. Kwani iwapo watapuuza wajue wanaanda mazingira ya kupuuzwa.

Alisema katika kufanikisha azima hiyo hawana budi waongeze ujuzi kupitia vyuo, mafunzo, semina na kubadilishana uzoefu na wanataaluma wenzao.

Alisema licha ya kuwafanya wathaminiwe, lakini pia kuongeza ujuzi kutasababisha kupanua wigo wa ajira na masilahi kupitia kazi yao ya uandishi.

Katika mkutano huo wanachama wa klabu ya waandishi wa habari wa mkoa wa Lindi walifanya marekebisho ya baadhi ya ibara na vifungu mbalimbali vya katiba ya klabu hiyo na kuunga mkono maazimio kumi ya Umoja wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC).

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments