SERIKALI YAKABIDHI VISHIKWAMBI 6600 KWA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt,Francis Michael (kulia) akimkabidhi vishikwambi Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Khamis Abdulla Said katika hafla ya makabidhiano ya vishikwambi 6600 kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar leo Desemba 22,2022 Jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt,Francis Michael (kulia) akimkabidhi vishikwambi Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Khamis Abdulla Said katika hafla ya makabidhiano ya vishikwambi 6600 kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar leo Desemba 22,2022 Jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt,Francis Michael akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya vishikwambi 6600 kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar leo Desemba 22,2022 Jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt,Francis Michael (katikati) akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya vishikwambi 6600 kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar leo Desemba 22,2022 Jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Khamis Abdulla Said akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya vishikwambi 6600 kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar leo Desemba 22,2022 Jijini Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya vishikwambi 6600 kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar leo Desemba 22,2022 Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya Wakurugenzi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wakifuatilia hafla ya makabidhiano ya vishikwambi 6600 kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar leo Desemba 22,2022 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*****************

EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekabidhi Vishikwambi 6600 kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kuwagawia walimu wa Shule za msingi na Sekondari ili kusaidia kuwarahisishia katika kufundisha.

Akizungumza leo Desemba 22, 2022 Jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla fupi ya Makabidhiano hayo Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt,Francis Michael amesema kuwa vishikwambi hivyo ni kati ya vile laki tatu vilivyotumika wakati wa sensa ya watu na Makazi ya mwaka huu ambapo baada ya kazi hiyo Serikali iliamua kuvigawa kwa walimu ili kuwasaidia katika ufanyaji wa kazi.

Amesema Vishikwambi 6600 vitapelekwa Zanzibar huku 2093 vilishagaiwa Tanzania bara tokea Novemba 4,2022 ambapo Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassimu Majaliwa alikuwa mggeni rasmi kwenye uzinduzi wa ugawaji wa vishikwambi hivyo.

"Vishikwambi hivi ni mali ya walimu na ni matarajio vitakuwa chachu katika kuboresha mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji ili kuinua ubora wa elimu hapa nchini na Visiwani". Amesema Dkt.Michael.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Khamis Abdulla Said ameahidi kufuata maelekezo ya Waziri Mkuu na havitakwenda kukaa stoo na badala yake wataenda kuvigawa kwa wahusika ambao ni walimu.

Aidha amesema kuwa kupokea kwa vishikwambi hivyo ni kama changamoto ya mabadiliko ya kwenda kwenye TTEHAMA hivyo walimu wa Zanzibar wawe tayari kuvitumia ipasavyo.

Hata hivyo amemshukuru Rais wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuunga mkono sekta ya elimu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post