OPE WASHIRIKI UZINDUZI UPANDAJI MITI SHINYANGA



Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi, akipanda mti katika uzinduzi wa zoezi la upandaji miti halmasshauri ya wilaya ya Shinyanga, uzinduzi uliofanyika Kata ya Mwalukwa Shule ya Msingi Ng'hama.



Mkurugenzi wa Shirika la OPE William Shayo, akipanda mti katika uzinduzi wa zoezi la upandaji miti halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, uzinduzi uliofanyika Kata ya Mwalukwa Shule ya Msingi Ng'hama.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA 

SHIRIKA la  Organisation Of People Empowerment (OPE) limeshiriki zoezi la uzinduzi wa upandaji miti katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na athari za mazingira.



Uzinduzi huo wa upandaji miti umefanyika leo Desemba 22,2022 katika shule ya Msingi Ng'hama iliyopo Kata ya Mwalukwa wilayani Shinyanga, huku Mgeni Rasmi akiwa ni Katibu Tawala wa wilaya hiyo Boniphace Chambi kwa niaba ya Mkuu wa wilaya Jasinta Mboneko.

Chambi akizungumza kwenye uzinduzi huo wa upandaji miti wilayani Shinyanga, ametoa wito kwa wananchi waitikie elimu ambayo wanapewa na Shirika la Ope na kupanda miti kwa wingi pamoja na kuitunza.

"Zoezi la upandaji miti halmashauri ya wilaya ya Shinyanga nimelizindua rasmi, nalipongeza pia Shirika la OPE kwa kuhamasisha na kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kupanda miti na faida zake," amesema Chambi.

"Naomba pia wananchi wapande miti kwenye maeneo ya mipaka yao, ili kutatua tatizo la migogoro ya ardhi,"ameongeza.

Naye diwani wa Kata ya Mwalukwa Ngassa Mboje, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, amelipongeza Shirika la OPE kwa kuanzisha Kitalu cha kupanda miche ya miti, na kuhamasisha wananchi kupanda miti kuwagawia bure, hali ambayo itasaidia kuwa na miti mingi na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Naye Afisa Miradi kutoka Shirika la OPE Laurent Mpuya, amesema Shirika hilo lilianzisha ujenzi wa kitalu cha miche June mwaka huu, na mradi wa kusambaza miche ya miti bure na kutoa elimu ya faida ya miti kwa wananchi, wanautekeleza katika Kata mbili Mwalukwa na Pandagichiza na wameshatoa miche 75,650.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Edward Maduhu, amesema halmashauri hiyo imepanga kupanda Miti milioni 1.5 kwa mwaka mzima, na kubainisha kuwa muitikio wa wananchi wa upandaji miti ni mzuri hasa kwenye kipindi cha msimu mvua, na katika uzinduzi huo wamepanda Miti 200.


Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi, akizindua upandaji Miti Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Diwani wa Mwalukwa Ngassa Mboje ambaye pia ni Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga akizungumza kwenye uzinduzi wa upandaji Miti wilayani humo.

Afisa Miradi kutoka Shirika la OPE Laurent Mpuya, akizungumza kwenye uzinduzi wa upandaji Miti Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi (kulia) akimkabidhi cheti cha pongezi Mkurugenzi wa Shirika la OPE William Shayo, kutokana na kazi kubwa ambayo wanaifanya ya kuhamasisha wananchi kupanda miti na kuwapatia miche bure.

Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi, akipanda Mti kwenye uzinduzi wa upandaji Miti Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Diwani wa Mwalukwa Ngassa Mboje ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga akipanda Mti kwenye uzinduzi huo.

Mkurugenzi wa Shirika la OPE William Shayo, akipanda mti katika uzinduzi wa zoezi la upandaji miti halmasshauri ya wilaya ya Shinyanga, uzinduzi uliofanyika Kata ya Mwalukwa Shule ya Msingi Ng'hama.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Edward Maduhu, akipanda Mti kwenye uzinduzi huo.

Afisa Miradi kutoka Shirika la OPE Laurent Mpuya akipanda Mti kwenye uzinduzi huo.

Mhifadhi wa Misitu TFS Medard Nonghorya akipanda Mti kwenye uzinduzi huo.

Kaimu Afisa Mtendaji wa Mwalukwa Elipendo John, ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mwalukwa akipanda Mti kwenye uzinduzi huo.

Zoezi la upandaji Miti likiendelea.

Zoezi la upandaji Miti likiendelea.

Zoezi la upandaji Miti likiendelea.

Zoezi la upandaji Miti likiendelea.

Zoezi la upandaji Miti likiendelea.

Zoezi la upandaji Miti likiendelea.
 

Zoezi la upandaji Miti likiendelea.

Zoezi la upandaji Miti likiendelea.

Muonekano wa Kitalu cha uoteshaji Miche ya Miti kutoka Shirika la OPE.

Muonekano wa Kitalu cha uoteshaji Miche ya Miti kutoka Shirika la OPE.

Kauli Mbiu ya Kampeni ya upandaji Miti kutoka Shirika la OPE.

Muonekano wa Kitalu cha uoteshaji Miche ya Miti kutoka Shirika la OPE.

Muonekano wa Kitalu cha uoteshaji Miche ya Miti kutoka Shirika la OPE.

Mkurugenzi wa Shirika la OPE William Shayo akiwa amebeba Miche ya Miti kwa ajili ya kwenda kuipanda.

Ubebaji Miche ya Miti ukiendelea kwa ajili ya kwenda kupandwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments