MAHAFALI YA KWANZA SHULE YA AWALI NA MSINGI SHADE YAFANYIKA SHINYANGA

Maandamano ya wahitimu wa darasa la awali yakiendelea kuelekea ukumbini.
 ***

Mahafali ya kwanza katika shule ya Awali na Msingi SHADE ‘Shade Pre and Primary School’ yamefanyika ambapo jumla ya wanafunzi 17 wavulana wakiwa 8 na wasichana 9 wamehitimu shule ya awali ‘Nursery’ tayari kabisa kwa kujiandaa na masomo ya darasa la kwanza mwaka 2023 katika Shule hiyo.

Mahafali hayo yamefanyika leo Jumatano Desemba 7,2022 katika shule ya Msingi Shade (Shade Pre and Primary School) iliyopo katika mtaa wa Magobeko kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.

Akisoma Risala, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Awali na Msingi SHADE, Lazaro Agustino Sibale amesema shule hiyo imeanzishwa mwaka 2021 ikiwa na jumla ya wanafunzi 21 wa kike 9 na wa kiume 12.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shade Pre and Primary School, Bw. John Isack Migila amesema lengo la kuanzishwa kwa Shule hiyo ni kutaka kutoa elimu bora na yenye kukaribia viwango vya kimataifa ikiwemo kuhakikisha mtoto anapata maarifa stahiki awapo katika mchakato wa ujifunzaji .

Amesema pia shule hiyo inatoa elimu bure kwa watoto wamakundi maalumu kama vile watoto wenye ualubino ,yatima na huku watoto wengine ambao wazazi wao wana uwezo wakilipa ada rafiki kwa ajili ya kuwezesha na kuendeleza shule hiyo.

Aidha amesema, katika kuhakikisha Shule inatoa elimu bora wanafunzi wanalelewa kiroho bila kubagua dini maana watoto wadini zote wanapokelewa katika shule hiyo bila kujali dini zao.

Kwa upande wake Afisa elimu Taaluma Manispaa ya Shinyanga Wingwira Kitila ambaye alikuwa Mgeni rasmi wakati wa mahafali hayo ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wazazi na walezi kulinda watoto na kufuatilia maendeleo ya watoto wao pindi wawapo shuleni na akiwasihi kujenga utamaduni wa kuripoti matukio ya vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watoto kwenye maeneo yao ili serikali iweze kuchukua hatua.
Mgeni rasmi Wingwila Kitila akizungumza na wazazi na walezi.
Mgeni rasmi Wingwila Kitila akizungumza na wazazi na walezi.
Mgeni rasmi Wingwila Kitila akizungumza na wazazi na walezi.
Mgeni rasmi Wingwila Kitila akizungumza na wazazi na walezi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shade Pre and Primary School,Bw. John Isack Migila akizungumza
Mkurugenzi Mtendaji wa Shade Pre and Primary School,Bw. John Isack Migila akizungumza
Maandamano ya wahitimu wa darasa la awali yakiendelea kuelekea ukumbini.
Maandamano ya wahitimu wa darasa la awali yakiendelea kuelekea ukumbini.
Maandamano ya wahitimu wa darasa la awali yakiendelea kuelekea ukumbini.
Wahitimu wakicheza pamoja na mwalimu wao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shade Pre and Primary School,Bw. John Isack Migila akijiandaa kukata utepe akiwa na wahitimu.
Mwalimu mkuu wa Shade ,mkurugenzi ,meneja wa shule pamoja na wageni waalikwa wakiwa kwenye picha ya pamoja wakiendelea na sherehe.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post