SIAGI AONGOZA MAPOKEZI YA MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WAZAZI CCM TAIFA FADHIL MAGANYAMwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga John Siagi (kulia) baada ya kumpokea Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na mjumbe wa kamati kuu Fadhil Maganya (katikati), kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Anord Makombe


***
Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga John Siagi ameongoza viongozi na wajumbe wachama hicho kumpokea Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na mjumbe wa kamati kuu Fadhil Maganya .


Mapokezi hayo ya kumpokea Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi Taifa Fadhil Maganya yamefanyika leo Jumatano Desemba 21,2022 katika ofisi za chama hicho ngazi ya mkoa na kuongozwa na mwenyekiti wa jumuiya ya Wazazi mkoani humo akiambatana na viongozi wengine wa chama na mkoa.


Mapokezi ya kumpokea kiongozi Maganya yameanzia Shule ya Msingi Buhangija na kuongozwa na vijana wa hamasa pamoja na bendi kuelekea katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Shinyanga.


Maganya amefika mkoani Shinyanga na kukutana na viongozi wa jumuiya hiyo ikiwa ni mara yake ya kwanza kufika mkoani humo tangu achaguliwe kuwa mwenyekiti wa jumuia ya Wazazi Taifa na mjumbe wa kamati kuu ambapo pamoja na mambo mengine amefanya mazungumzo na viongozi wote wa jumuia hiyo kuanzia ngazi ya Mtaa hadi mkoa .


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na mjumbe wa kamati kuu Fadhil Maganya akitoa salamu zake kwa uongozi wa chama na jumuiya ya wazazi ameeleza kuwa amepita kusalimia ikiwa ni sehemu ya safari yake kuelekea mkoani Mara kwa ajili ya ziara.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na mjumbe wa kamati kuu Fadhil Maganya akisaini kitabu cha wageni katika ukumbi mdogo wa CCM Mkoa.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na mjumbe wakamati kuu Fadhil Maganya akiingia ukumbini na mwenyeji wake Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi mkoa wa Shinyanga John Siagi (kushoto)
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na mjumbe wa kamati kuu Fadhil Maganya akisalimiana na viongozi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post