KARIBU TANZANIA ORGANIZATION, TAKUKURU, BUHANGIJA FDC WATOA ELIMU YA KUPINGA RUSHWA YA NGONO KWA WAENDESHA BAISKELI NA WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA

Mkurugenzi wa Shirika la Karibu Tanzania Organization, Maggid Mjengwa akizungumza wakati wa mafunzo ya kupinga Rushwa ya Ngono kwa Waendesha Baiskeli na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Shirika lisilo la Kiserikali la Karibu Tanzania Organization (KTO) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Buhangija mkoani Shinyanga limetoa elimu ya kupinga Rushwa ya Ngono kwa Waendesha Baiskeli na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga.

Mafunzo hayo yamefanyika leo Ijumaa Desemba 16,2022 katika ukumbi wa shule ya Msingi Buhangija Manispaa ya Shinyanga ambapo Waendesha baiskeli kupitia chama cha waendesha baiskeli mkoa wa Shinyanga na Waandishi wa habari wamepewa mafunzo kuhusu namna ya kukabiliana na rushwa ya ngono.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Shirika la Karibu Tanzania Organization, Maggid Mjengwa amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari na waendesha baiskeli kuhusu masuala ya rushwa ya ngono ili wawe mabalozi wa kupinga rushwa ya ngono ikiwa ni sehemu ya kutekeleza kauli mbiu yetu ya ‘Kuwa Jasiri Kataa ya Rushwa ya ngono’.

“KTO tunafanya kazi kwa ukaribu sana na wadau mbalimbali katika kupambana na masuala ya rushwa ya ngono. Tunatoa elimu ya kupinga rushwa kwenye vyuo 54 vya maendeleo ya wananchi ‘FDCs’. Waandishi wa habari mkiwa na uelewa mtasambaza elimu hii ili kuisaidia jamii, nanyi waendesha baiskeli mtakuwa mabalozi wazuri wa kufikisha elimu ya kupambana na rushwa ya ngono katika jamii”,amesema Mjengwa.
Mkurugenzi wa Shirika la Karibu Tanzania Organization, Maggid Mjengwa.

“Suala la Rushwa kila mmoja linamhusu hivyo ni lazima ashiriki kutokomeza rushwa ya ngono. Elimu tulitoa leo ni sehemu ya maandalizi ya Uzinduzi wa Kampeni ya Miezi mitatu ya kutoa elimu kupinga rushwa ya ngono ambapo kwa upande wa Shinyanga uzinduzi utafanyika Desemba 17,2022 katika uwanja wa CCM Kambarage”, ameongeza Mjengwa.

Afisa Uchunguzi TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga, Reuben Chongolo amesema Mapambano ya rushwa yanawezekana endapo tu kila mmoja atazingatia maadili na kuwa waadilifu, sheria kanuni na taratibu.

“Vyanzo vya rushwa ni pamoja na mmomonyoko wa maadili, tama ya mwili, kutokujua haki na wajibu, kutojiamini kutokana na kukosa sifa na tama ya kupata au kujihakikishia huduma haraka na madhara ya rushwa ya ngono ni ukiukwaji wa haki za binadamu, ukiukwaji wa utawala wa sheria na taratibu za kazi, kuajiriwa watu wasio na sifa, kuzorotesha utendaji kazi wa taasisi na kupatikana kwa wasomi wenye uwezo duni”,amesema Chongolo.

Ameyataja Madhara mengine ya rushwa ya ngono kuwa ni kukatisha masomo hasa kwa wasichana wa shule na vyuo, kuwepo kwa mahusiano mabaya kati ya mwajiri na mwajiriwa, kuongezeka kwa maambukizi ya magonjwa ya zinaa ukiwemo UKIMWI na mimba zisizotarajiwa hali inayochangia kuongezeka kwa watoto mitaani.
Afisa Uchunguzi TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga, Reuben Chongolo.

“Ukizuia rushwa ya ngono unalinda utu wa mwanamke , utafanya haki itendeke. Kwa pamoja tunaweza kutokomeza rushwa ya ngono kama zilivyo rushwa nyingine, wananchi wote kwa pamoja tunatakiwa kushirikiana kwa kutoa taarifa katika ofisi ya TAKUKURU. Wananchi na watumishi katika maeneo ya kazi wanatakiwa kuachana na vishawishi ambavyo vitawaingiza katika vitendo vya rushwa kwa kuzingatia maadili na kanuni za kazi”,ameongeza Chongolo.

Kwa upande wake, Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Bi. Mwamba Masanja amewataka wanaume kuvunja ukimya kuhusu vitendo vya rushwa kwani yanaathiri taifa.

“Suala la rushwa linaathiri nchi, kila mmoja anatakiwa kupinga rushwa siyo hii ya ngono tu”,amesema Masanja.

Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Buhangija Bi. Maria Mkanwa amewashauri wanawake vijana waliokatisha masomo kwa sababu yoyote ile kuchangamkia fursa ya Programu ya Elimu Haina Mwisho ambayo inatolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana Shirika la KTO na vyuo vya maendeleo ya wananchi – FDCs.
Mkuu wa Chuo cha Buhangija FDC Bi. Maria Mkanwa.

“Elimu Haina Mwisho ni Programu maalumu ya kuendeleza maarifa kwa wanawake vijana waliokatishwa masomo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ujauzito pamoja na wale ambao hawakupata nafasi ya kuendelea na masomo ya sekondari”,ameeleza Mkanwa.

“Ukijiunga na Programu hii utasoma masomo ya sekondari kupitia mfumo usio rasmi, masomo ya ufundi, ujasiriamali na stadi za maisha. Kozi hii inatolewa bure. Mshiriki hatalipia ada ya masomo, chakula wala hosteli kwani vyote vinagharamiwa na serikali lakini mshiriki atajitegemea kwa mahitaji yake binafsi. Kwa wale wa kutwa (wanaokwenda na kurudi) ambao wana watoto wadogo watapata huduma ya Day Care iliyopo chuoni bure”,ameongeza Mkanwa.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkurugenzi wa Shirika la Karibu Tanzania Organization, Maggid Mjengwa akizungumza wakati wa mafunzo ya kupinga Rushwa ya Ngono kwa Waendesha Baiskeli na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Desemba 16,2022. Kushoto ni Afisa Uchunguzi TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga, Reuben Chongolo akifuatiwa na Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Bi. Mwamba Masanja, Kulia ni Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Buhangija Bi. Maria Mkanwa. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Shirika la Karibu Tanzania Organization, Maggid Mjengwa akizungumza wakati wa mafunzo ya kupinga Rushwa ya Ngono kwa Waendesha Baiskeli na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga
Mkurugenzi wa Shirika la Karibu Tanzania Organization, Maggid Mjengwa akizungumza wakati wa mafunzo ya kupinga Rushwa ya Ngono kwa Waendesha Baiskeli na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga
Mkurugenzi wa Shirika la Karibu Tanzania Organization, Maggid Mjengwa akizungumza wakati wa mafunzo ya kupinga Rushwa ya Ngono kwa Waendesha Baiskeli na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Buhangija Bi. Maria Mkanwa akizungumza wakati wa mafunzo ya kupinga Rushwa ya Ngono kwa Waendesha Baiskeli na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga

Afisa Uchunguzi TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga, Reuben Chongolo akitoa elimu ya madhara ya Rushwa wakati wa mafunzo ya kupinga Rushwa ya Ngono kwa Waendesha Baiskeli na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga

Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Bi. Mwamba Masanja akitoa elimu ya madhara ya Rushwa wakati wa mafunzo ya kupinga Rushwa ya Ngono kwa Waendesha Baiskeli na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga

Afisa Habari wa Shirika la Karibu Tanzania Organization Bi. Symphrose Makungu akizungumza wakati wa mafunzo ya kupinga Rushwa ya Ngono kwa Waendesha Baiskeli na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga
Afisa Habari wa Shirika la Karibu Tanzania Organization Bi. Symphrose Makungu akizungumza wakati wa mafunzo ya kupinga Rushwa ya Ngono kwa Waendesha Baiskeli na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga
Washiriki wa mafunzo ya kupinga rushwa ya ngono wakiwa ukumbini.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments