MAMLAKA YA HALI YA HEWA IMEKAMILISHA UTENGENEZAJI MITAMBO YA RADA MBEYA, KIGOMAMkurugenzi wa huduma za utabiri wa Hali ya hewa Tanzania Dk. Hamza Kabelwa akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dodoma katika ukumbi wa Idara ya Habari-maelezo

Na Dotto Kwilasa, DODOMA.


Mamlaka ya hali ya hewa nzania (TMA)imesema  imekamilisha kwa asilimia 90 utengenezaji wa mitambo ya rada mbili mkoani MbeyTanzania a na Kigoma na sasa  ina rada tatu zilizopo katika Jiji la Dar es Salaam, Mwanza na Mtwara ambazo zinafanya kazi ya kukusanya data za hali ya hewa zinazoonesha uhalisi wa anga la Tanzania.


Akizungumza Jijini Dodoma, Mkurugenzi wa huduma za utabiri wa hali ya hewa Tanzania, Dk Hamza Kabelwa amesema mwaka 2021/22, mamlaka hiyo imeendelea na utekelezaji wa mradi huo wa rada, vifaa na miundombinu ya hali ya hewa ambazo hatua mbalimbali zimefikiwa.

 

“Ujenzi wa miundombinu ya rada za Mbeya na Kigoma pamoja na malipo ya asilimia 90 ya rada hizo yalifanyika,” amesema.


Pia mafunzo kwa wahandisi na waendesha mitambo kuhusu kuzihudumia na kuzitumia rada hizo yalifanyika kiwandani nchini Marekani.


Dk Kabelwa amesema, mamlaka hiyo katika mwaka huo 2021/22 iliendelea na utengenezaji wa rada mbili zitakazofungwa katika Kiwanja cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA) na Jijini Dodoma umefikia asilimia 45. 


"Mamlaka ya TMA ilifungua barua za dhamana kwa ajili ya malipo ya asilimia 80 ya kutengeneza rada ambapo kukamilika kwa rada hizi kutakamilisha mtandao wa rada nchini wa kuwa na idadi ya rada saba,"amesema.


Dk Kabelwa amesema, rada hizo zina uwezo wa kuona zaidi ya kilometa za mkato 450 huku zikizunguka na kuona matone madogo  ya mvua katika hali ya uhalisia ndani ya kilometa 250.


Katika hatua nyingine amesema kwa mwaka wa fedha 2022/23 mamlaka hiyo imeweka mkakati wa kuendelea kutoa huduma ya hali ha hewa nchini kwa kupanua uwigo wa utoaji elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa hali ya hewa.


"Tunaendelea kukamilisha ukarabati wa majengo ya chuo cya hali ya hewa Kigoma, na ukarabati wa vituo vya hali ha hewa vinane vilivyopo Singida, Songwe, Dodoma, Tabora, Mpanda, Mahenge, Songea na Shinyanga.


Hatua hiyo itaimarisha uangazi wa hali ya hewa katika bahari na maziwa makuu na kuimarisha usalama wa abiria kwenye maji, shughuli za uvuvi pamoja na kusaidia shughuli mbalimbali zikiwemo za upakiaji mizigo banadarai na uvunaji wa gesi asilia,"amefafanua.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post