KAWAIDA ACHAGULIWA KWA KISHINDO KUWA MWENYEKITI WA UMOJA WA VIJANA WA CCM TAIFA 'UVCCM'


Wajumbe wa mkutano mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wamemchagua Mohamed Ali Mohammed (Kawaida) kuwa mwenyekiti mpya wa umoja huo.


Kawaida ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Kusini Unguja anachukua nafasi ya Kheri James ambaye Juni 2021 Rais Samia Suluhu Hassan alimteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo.


Kawaida amepata kura 523 akiwashinda Farid Mohammed Haji aliyepata kura 25, Kassim Haji Kassu kura 2 na Abdallah Ibrahim Natepe aliyepata kura 1.

Via Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments