SPIKA WA BUNGE LA AFRIKA KUSINI : NCHI ZA AFRIKA TUNAPIGA HATUA NZURI KATIKA KUWAPA NAFASI ZA UONGOZI WANAWAKE


Spika wa Bunge la Serikali ya Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Mapisa Nqakula kwenye Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge la Afrika juu ya Haki za Wanawake.


Na Kadama Malunde - Midrand Afrika Kusini
Spika wa Bunge la Serikali ya Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Mapisa Nqakula amesema Bara la Afrika limepiga hatua kubwa katika kuwapa nafasi wanawake kwenye nafasi za uongozi.


Mhe. Nqakula amesema hayo leo Ijumaa Novemba 4,2022 kwenye Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge la Afrika juu ya Haki za Wanawake unaoendelea katika ukumbi wa Bunge la Afrika Midrand Afrika Kusini ukiongozwa na mada ‘Uwezeshaji na ushirikishwaji wa wanawake katika utawala’.

"Ni lazima tutambue kwamba maendeleo mengi yamefanywa na bara la Afrika, sio tu kubadili athari za ukosefu wa usawa wa kijinsia, lakini pia kujitayarisha kufaidika na faida ya kuongezeka kwa ushiriki wa wanawake katika uongozi na katika uchumi",amesema.


Amesema kwa miaka mingi tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Afrika, bara la Afrika limeonyesha dhamira ya kukuza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake.


"Tumeshuhudia kuongezeka kwa uwakilishi na ushiriki katika ngazi za kufanya maamuzi. Viongozi wa nchi za Afrika wameonyesha dhamira ya kweli kulelta usawa wa kijinsia. Tunashukuru Barani tunaendelea kufanya vizuri katika kuwapa wanawake nafasi za uongozi. Sisi wanawake tunafanya kazi vizuri, Tumeona katika siasa idadi ya wanawake inaongezeka mfano tuna idadi kubwa ya wanawake maspika wa bunge kwenye nchi zetu”,amesema Mhe. Nqakula.

“Pia ni vyema wanawake washirikishwe katika masuala ya amani kwani panapotokea vurugu wanaoathirika zaidi ni wanawake na watoto, wanaoumia zaidi ni wanawake lakini pia bado wanawake hawajajumuishwa sana katika masuala ya uchumi.

Usawa wa kijinsia unahitaji utashi wa kisiasa, ni jukumu la wabunge kuhakikisha wanasimamia masuala ya usawa kijinsia yanapewa kipaumbele ili kuhakikisha kuwa wanawake hawatengwi hivyo wanawake wawe kwenye tabaka la watu wengi”,amesema.


Hata hivyo amesema hali za maisha za wanawake bado hazijaboreshwa, wanawake wanaajiriwa katika nafasi za chini na hata mishahara wanayolipwa wanawake na wanaume tofauti ni kubwa.


"Tunataka pia kuona idadi ya wanawake inaongezeka katika bodi za Mashirika na Makampuni. Ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha kuna usawa wa kijinsia katika kila eneo",ameongezaa Mhe. Nqakula.
Spika wa Bunge la Serikali ya Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Mapisa Nqakula kwenye Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge la Afrika juu ya Haki za Wanawake. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Spika wa Bunge la Serikali ya Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Mapisa Nqakula kwenye Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge la Afrika juu ya Haki za Wanawake.
Spika wa Bunge la Serikali ya Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Mapisa Nqakula kwenye Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge la Afrika juu ya Haki za Wanawake.
Makamu wa Rais wa Tatu wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament - PAP), Mhe. Lucia Doss Passos akizungumza wakati wa Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge la Afrika juu ya Haki za Wanawake
Makamu wa Rais wa Tatu wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament - PAP), Mhe. Lucia Doss Passos (kulia) akizungumza wakati wa Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge la Afrika juu ya Haki za Wanawake

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments