WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA WAANZA MBIO KUTEKELEZA MRADI WA SAUTI ZA KAYA NA VYOMBO VYA HABARI KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO

Mratibu wa Mfuko wa wanawake Tanzania (WFT-T) Mkoa wa Shinyanga wa Shinyanga Glory Mbia akizungumza wakati wa mafunzo elekezi kwa waandishi wa habari kuhusu ufuatiliaji wa matokeo ya Mpango Mkakati wa Kupunguza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA). Picha na Kadama Malunde 
Mratibu wa MTAKUWWA ambaye ni Ofisa Maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Aisha Omary(aliyevaa ushungi), Paschalia Mbugani kutoka Shirika la Thubutu Africa (wa pili kulia waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na Waandishi wa Habari wanaotekeleza mradi wa "Sauti za Kaya na Vyombo vya Habari katika Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto". 

Na Frank Mshana ,Shinyanga

KLABU ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga ( Shinyanga Press Club - SPC) mafunzo elekezi kwa waandishi wa habari 15 juu ya kufuatilia matokeo ya Mpango Mkakati wa Kupunguza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA).

Mafunzo hayo yamefanyika leo Novemba 26, 2022 katika Manispaa ya Shinyanga kwa ufadhili wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (WFT-Trust) katika hatua ya utekelezaji wa mradi wa awamu ya tatu unaoitwa "SAUTI ZA KAYA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO".

Mradi huo utatekelezwa kwa kipindi cha miezi mitatu katika eneo la halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwenye kata 15 zilizolengwa.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mwezeshaji  Paschalia Mbugani kutoka Shirika la Thubutu Africa Initiative (TAI) la mkoani Shinyanga amesema wadau wengi wametekeleza afua za MTAKUWWA na yapo baadhi ya matokeo ya awali ambapo vyombo vya habari vinawajibu wa kufanya tathimini juu ya madiliko hayo.

"Vyombo vya habari ni jicho pekee la kuweza kupima mabadiliko hayo ndani ya jamii baada ya wadau wa kupinga ukatili kutekeleza afua zao", amesema Mbugani.

Mratibu wa  Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC) ambaye ni Mratibu mradi huo Estomine Henry amesema hii ni awamu ya tatu katika kufanya mradi huu wa masuala ya ukatili ana imani waandishi wa habari watafanya vizuri zaidi.

“Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga mmekuwa mkifanya vizuri katika mradi yote ya kupinga ukatili hivyo mradi huu ni mwendelezo wa kufanya vizuri zaidi”, amesema Henry.

Makamu Mwenyekiti wa SPC, Patrick Mabula amewataka waandishi wa habari wafanye kazi za mradi huu kwa juhudiili wanatetea haki za wanawake na watoto.

Baadhi ya waandishi wa habari akiwemo Suzy Butondo na Amos John wamesema changamoto kubwa iliyokuwepo kwenye miradi iliyopita ni kukosa ushirikiano kwa baadhi ya watendaji wa kata kwa kuogopa vyombo vya habari jambo ambalo nao wanatakiwa wapewe elimu ili watoe ushirikino.

Mratibu wa Mfuko wa wanawake Tanzania (WFT-T) Mkoa wa Shinyanga wa Shinyanga Glory Mbia amesema wanaitambua Shinyanga Press Club (SPC) kama mdau muhimu katika kutetea haki za wanawake na watoto na inafanya kazi vizuri na kuibua changamoto zinazosababisha vitendo vya ukatili katika jamii hali ambayo wameitaja kuwa imesaidia kupunguza vitendo hivyo huku Serikali ikendelea kulitambua kundi la Wanahabari kama mdau muhimu wa maendeleo ya jamii.

“Vyombo ya habari ni mkono wenye nguvu wa kuleta mabadiliko kwa jamii na serikali ikiwa watazingatia misingi ya taalauma yao katika kutetea haki za wanawake na watoto ambao hawapati haki ya kutoa taarifa zao kupitia mifumo iliyowekwa na serikali”,amesema Mbia.

Mratibu wa MTAKUWWA ambaye ni Ofisa Maendeleo ya jamii kutoka halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Aisha Omary amesema serikali itatoa ushirikiano wa kutosha kwa waandishi wa habari katika kutekeleza mradi huo.

“Nawaombeni popote mtakapopata changamoto ya watumishi wenzangu kwenye kata za mradi kwa kutopata ushirikiano tuwasiliane”,amesema Omary.
Mratibu wa MTAKUWWA ambaye ni Ofisa Maendeleo ya jamii kutoka halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Aisha Omary akizungumza leo Jumamosi Novemba 26,2022 wakati wa mafunzo elekezi kwa waandishi wa habari kuhusu ufuatiliaji wa matokeo ya Mpango Mkakati wa Kupunguza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA). Kushoto ni Mratibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC), Estomine Henry, kulia ni Mwezeshaji wa mafunzo hayo Paschalia Mbugani kutoka Shinyanga la Thubutu Africa. Picha na Kadama Malunde
Mratibu wa MTAKUWWA ambaye ni Ofisa Maendeleo ya jamii kutoka halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Aisha Omary akizungumza leo Jumamosi Novemba 26,2022 wakati wa mafunzo elekezi kwa waandishi wa habari kuhusu ufuatiliaji wa matokeo ya Mpango Mkakati wa Kupunguza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA).

Makamu Mwenyekiti wa SPC, Patrick Mabula akizungumza wakati wa mafunzo elekezi kwa waandishi wa habari kuhusu ufuatiliaji wa matokeo ya Mpango Mkakati wa Kupunguza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA). Kulia ni Mratibu wa MTAKUWWA ambaye ni Ofisa Maendeleo ya jamii kutoka halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Aisha Omary, Kushoto ni Mratibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC), Estomine Henry. 
Makamu Mwenyekiti wa SPC, Patrick Mabula akizungumza wakati wa mafunzo elekezi kwa waandishi wa habari kuhusu ufuatiliaji wa matokeo ya Mpango Mkakati wa Kupunguza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA).
Mratibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC), Estomine Henry akielezea kuhusu  Mradi wa "SAUTI ZA KAYA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO" unaotekelezwa na SPC  kwa ufadhili wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (WFT-Trust).

Mratibu wa Mfuko wa wanawake Tanzania (WFT-T) Mkoa wa Shinyanga wa Shinyanga Glory Mbia akizungumza wakati wa mafunzo elekezi kwa waandishi wa habari kuhusu ufuatiliaji wa matokeo ya Mpango Mkakati wa Kupunguza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA).

Mwezeshaji, Paschalia Mbugani kutoka Shirika la Thubutu Africa Initiative (TAI) la mkoani Shinyanga akizungumza wakati wa mafunzo elekezi kwa waandishi wa habari kuhusu ufuatiliaji wa matokeo ya Mpango Mkakati wa Kupunguza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA).

Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.

Mwandishi wa habari wa Star Tv, Elizabeth Charles Nyanda akiandika dondoo muhimu
Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.

Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.
Mratibu wa MTAKUWWA ambaye ni Ofisa Maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Aisha Omary(aliyevaa ushungi), Paschalia Mbugani kutoka Shirika la Thubutu Africa (wa pili kulia waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na Waandishi wa Habari wanaotekeleza mradi wa "Sauti za Kaya na Vyombo vya Habari katika Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto".
Mratibu wa MTAKUWWA ambaye ni Ofisa Maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Aisha Omary(aliyevaa ushungi), Paschalia Mbugani kutoka Shirika la Thubutu Africa (wa pili kulia waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na Waandishi wa Habari wanaotekeleza mradi wa "Sauti za Kaya na Vyombo vya Habari katika Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto".

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post