TPDC YATEMBEZA MKONG'OTO SHIMUTA TANGA


Kikosi cha kuvuta kamba cha timu ya TPDC Wanaume wakiwa uwanjani wakijiindaa na mchezo dhidi ya TBS ambapo TPDC waliibuka na ushindi wa mivuto 2-0.


Na Oscar Assenga,TANGA

TIMU ya mchezo wa kuvuta kamba ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa upande wa wanawake leo wamefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Michuano ya Shimuta baada ya kuivuta IRDP mivuto 2-0


Mchezo huo ambao ulikuwa wa kusisimua kutokana na kila timu kutaka kupata matokeo kwenye mtanange huo na hivyo timu ya TPDC kupambana vililvyo kuhakikisha wanaondoka na alama tatu kwenye mchezo huo .

Kwa kuonyesha kwamba wamedhamiria kunyakua vikombe kwenye michuano hiyo halikadhalika kwa upande wa wanaume waliweza kuibamiza timu ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kuwavuta mivuto 2-0 na hatimaye kutinga kwenye hatua hiyo.

Wakati huo huo timu ya Shirika hilo la Mpira wa Miguu imeibamiza timu ya TMDA bao 1-0 katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Sahare Jijini Tanga .

Bao pekee la TPDC lilifungwa na mshambuliaji wake machachari Phinias Ademba dakika ya 28 ambaye alitumia uzembe wa mabeki kupachika wavuni bao hilo.

Baadhi ya wachezaji wa Kikosi cha TPDC ambacho kilicheza dhidi ya TMDA ni Nahodha Dalushi Shija,Mshambuliaji Sem Shemzigwa,Midfielder Yusuph Juma,Phinias Ademba.

Timu ya kuvuta kamba ya TPDC kwa upande wa wanaume iliongozwa na Nahodha wake Joram Ndalahwa,Fransisco Masungulwa,Fidelis Mkiramweni huku kwa upande wa wanawake waliongozwa na Fatina Kagambo,Joyce Kiheka ambaye ni nahodha na Vick Patrick.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post