MASELE ATIA FORA HARAMBEE, ACHANGISHA MILIONI 62 KUNUNUA BASI LA KWAYA YA AIC SHINYANGA, APEWA TUZO


Mhe. Stephen Masele akionesha tuzo baada ya kukabidhiwa na uongozi wa kwaya kwa lengo la kutambua mchango wake na ushiriki wake katika harambee hiyo.

*****
Aliyekuwa Makamu wa kwanza wa Rais Bunge la Afrika na Mbunge mstaafu wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele leo Jumapili Novemba 13,2022 katika Kanisa la AICT KAMBARAGE SHINYANGA ameongoza harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ununuzi wa Basi ambapo amefanikiwa kuchangisha jumla ya shillingi 62,057,300/- (Sh. Milioni 62).


Akizungumza katika hafla hiyo Masele amewashukuru wananchi na waumini wa Kanisa la AICT Shinyanga kwa kuendelea kumkumbuka na kumshirikisha katika shughuli za kijamii hususani za kanisa huku akinukuu kitabu kitakatifu biblia Mithali 8: 17-21, amemshukuru Mungu kwa neema zake na kwa upendo mkubwa kwa taifa letu.


Mhe. Masele amewaomba waumini na wakristo kumuombea mhe Rais Samia Suluhu Hassan, “Tumuombee mama yetu na Rais wetu maisha marefu na afya njema azidi kutuongoza kwa hekima na busara, pia naomba waumini muendelee kuliombea taifa amani, utulivu na upendo".


Mhe. Stephen Masele ametunukiwa Tuzo ya upendo na Kanisa hilo na kumpongeza kwa uaminifu na upendo mkubwa kwa wana Shinyanga.


Akizungumza Mwenyekiti wa kwaya hiyo, Kambira Mtebe amemsifu Masele akisema ni kiongozi mnyenyekevu asiyekuwa na makuu, asiyependa majivuno. “Masele ni msikivu na mpole mwenye upendo sana, anawapenda sana watu”.


Naye Mlezi wa kwaya hiyo Abel Majige ambaye pia ni mmiliki wa Hotel ya Vigmark manispaa ya Shinyanga amemsifu Masele na kusema ni “kiongozi wa watu, Masele ni mtu wa watu” , amesema Majige.
Mhe. Stephen Masele akionesha tuzo baada ya kukabidhiwa na uongozi wa kwaya kwa lengo la kutambua mchango wake na ushiriki wake katika harambee hiyo
Mh. Stephen Masele akiwashukuru viongozi wa kwaya na kanisa kwa kumualika.
Mhe. Stephen Masele akikata
Mchungaji Magembe akitoa neno la shukrani baada ya zoezi la harambee hiyo kukamilika.
Uongozi wa kanisa ukimkabidhi tuzo mhe. StephenMasele .
Uongozi wa kanisa kwa niaba ya kwaya ukionesha tuzo iliyoandaliwa.
Zoezi la kuhesabu pesa zilizopatikana likiendelea.
Mwenyekiti wa kwaya Kambira Mtebe akimpongeza Mh.Masele.
Mh. Masele akifatilia harambee.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments