WHO NA SERIKALI KUSHIRIKIANA MIFUMO YA AFYA MKOANI KAGERA


*************** 

MBUNGE viti maalumu kupitia tiketi cha Chama cha Mapinduzi CCM Neema Lugangira amekutana na Dr. Domenti Oxana Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) katika Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU Commission) Jijini Berlin nchini Ujerumani tarehe 17 Oktoba na kufanya mazungumzo mbalimbali kwenye masuala ya kuboresha afya na siku ya tarehe 30 Oktoba kutakuwa na Kikao kingine Jijini Dar Es Salaam kitakachozungumzia mashirikiano baina ya WHO katika kuimarisha mifumo ya afya mkoani Kagera.

Washiriki wengine katika kikao hicho mbali na Lugangira(MB) ni pamoja na Toba Nguvila, Katibu Tawala Kagera, Dr Galbert Fedjo kutoka Ofisi ya Tanzania ya shirika la afya ulimwenguni (WHO) Dr Nathanael Sirili pamoja na Caroline Bollars ambaye ni Mtafiti kutoka Chuo kikuu cha Muhimbili (MUHAS) 

Mshauri Mwandamizi wa Ofisi ya WHO ndani ya Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) kutoka Brussels, Ubelgiji. 

Kikao kimekuwa na mafanikio makubwa sana. #KaziIendelee 🇹🇿

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post