WAZIRI DKT MABULA AWATAKA WAKURUGENZI HALMASHAURI KWENDA NA KASI YA RAIS SAMIA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza wakati wa kuhitimisha Kikao kazi kilichowaunganisha wakurugenzi wa Halmashauri na watalaam wa Sekta ya Ardhi nchini kilichofanyika jijini Dodoma Oktoba 1, 2022. Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Dkt Allan Kijazi na kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais –TAMISEMI Prof Riziki Shemdoe.

Sehemu ya washiriki wa kikao kazi kilichowaunganisha wakurugenzi wa Halmashauri na watalaam wa Sekta ya Ardhi nchini kilichofanyika jijini Dodoma Oktoba 1, 2022.

******************************

Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo yaMakazi Dkt Angeline Mabula amezitaka halmashauri nchini kwenda na kasi ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutenga ardhi kwa ajili ya uwekezaji.

Dkt Mabula alitoa kauli hiyo oktoba 1, 2022 wakati akihitimisha kikao kazi baina ya wakurugenzi wa halmashauri na wataalamu wa sekta ya ardhi kikichofanyika jijini Dodoma.

Huku akimshukuru Mhe Rais Samia kwa kuipa kipaumbele sekta ya ardhi, Dkt Mabula aliwaeleza washiriki wa kikao kazi kuwa, kinachohitajika kwa sasa ni kwenda na kasi ya mhe Rais hasa kwa kuzitaka halmashauri kujiandaa katika zoezi zima la uwekezaji.

"Hata kama mmetenga maeneo je meyatwaa na ni ya kwenu au mkipata muwekezaji ndiyo mnaanza kuhangaika, hapa kinachohitajika ni kwenda na kasi ya mhe rais na wakurugenzi ndiyo ninyi na maafisa ardhi ndiyo ninyi". Alisema Dkt Mabula

Aliongeza kwa kusema kuwa, ardhi zilizotengwa kwa ajili ya uwekezaji katika halmashauri, wakurugenzi wake wahakikishe wanazitwaa na kuwa mali ya serikali ili iwe rahisi kumpatia Muwekezaji pale anapotokea.

Aidha, Waziri wa Ardhi alizungunzia suala la halmashauri kushililia ardhi kwa muda mrefu bila kulipa fidia kwa wamiliki wake ambapo alisema pale halmashauri inaposhindwa kulipa fidia eneo ililotwaa basi eneo hilo lirudishwe kwa mhusika na pale litakapohitajika ufanyike tena uthamini.

" Kuna ardhi mmezihold kwa miaka nenda rudi fidia hailipwi lakini mgogoro unakuja ardhi sasa tuseme ukishindwa kulipa fidia maana hiyo ardhi umrudishie mwenyewe ukitaka tena utafanya uthamini" alisema Dkt Mabula

Aliwaambia washiriki wa mkutano huo kuwa, serikali haitaki uonevu kwa wananchi kwa kuwa siyo maelekezo ya rais na kusisitiza kuwa serikali inathamini wawekezaji hata wa ndani na pale wanapokuja wawekezaji wa nje wale wa ndani wasionekani siyo lolote.

Kikao kazi kati ya wakurugenzi wa halmashauri na wataalamu wa sekta ya ardhi mbali na mambo mengine kilijadili changamoto na kutoa maoni na ushauri kuhusu namna bora ya kusimamia watumishi wa sekta ya ardhi nchini kwa lengo la kuwa na ufanisi na kwa maskahi mapana ya nchi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post