SHIRIKA LA ADD INTERNATIONAL LATOA VIFAA WEZESHI "LAPTOP" KWA MASHIRIKA YANAYOJIHUSISHA NA WATU WENYE ULEMAVU SHINYANGA

Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Shinyanga Lidya Kwesigabo, (wa pili kulia) akimkabidhi mmoja wa viongozi wa Taasisi ya Amani Kopyuta Mpakato (Laptop) kwa ajili ya kumrahisishia katika majukumu yake kuwa hudumia watu wenye ulemavu, (kulia) ni Meneja wa mradi wa elimu jumuishi kutoka Add International Adam Mkaka

Na Abel Michael, SHINYANGA

SHIRIKA la Add International limetoa vifaa wezeshi (Laptop) kwa mashirika ambayo yanajihusisha na watu wenye ulemavu Mkoa wa Shinyanga, ili kuwaboreshea utendaji kazi kwa ufanisi pamoja na utunzaji wa kumbukumbu.

Vifaa hivyo wezeshi Kopyuta Mpakato zimetolewa leo Oktoba 18, 2022 kwenye Ofisi za Shirika la ADD International.

Meneja Mradi wa Elimu Jumuishi kutoka Shirika la ADD Intenational Adam Mkaka, amesema wametoa vifaa hivyo wezeshi Kopyuta Mpakato (Laptop) kwa mashirika ambayo yanajihusiha na watu wenye ulemavu, ili kuwaboreshea ufanisi wa utendaji kazi pamoja na kutunza kumbukumbu zao za ofisi vizuri.

Amesema mipango ya Shirika hilo ni kuungana na mashirikia mengine katika kutetea haki za watu wenye ulemavu, pamoja na kuhakikisha watoto wenye ulemavu wanapata haki yao ya kusoma na kuacha kunyanyapaliwa ili kutimiza ndoto zao, na ndiyo maana wametoa vifaa hivyo wezeshi kwa mashirika ambayo yanajihusisha na watu wenye ulemavu ili wakafanye kazi zao kwa ufanisi.

"Tafiti zinaonyesha Mikoa ya Kanda ya Ziwa imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya watoto wenye ulemavu kutopelekwa shule, hivyo lengo la mradi huu ni kuhakikisha watoto wote wenye ulemavu wanaandikishwa na kuanza shule mara moja,"amesema Mkaka.

"Leo Shirika letu la ADD Intenational tumetia saini na kukabidhi kopyuta mpakato kwa mashirika ambayo yanajihusisha na watu wenye ulemavu, ili kuongeza chachu katika utendaji wao wa kazi na kuhakikisha jamii inaongeza uelewa kwenye masuala yanayohusu watu wenye ulemavu, na kuacha tabia ya kuwanyanyapaa pamoja na kuwapeleka watoto shule,"ameongeza.

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Shinyanga Lidya Kwesigabo, ameyataka Mashirika yaliyopewa vifaa hivyo kwenda kuvitumia kikamilifu kwa malengo yaliyokusudiwa na kuleta matokeo chanya.

Nao baadhi ya Washiriki kutoka kwenye mashirika hayo akiwamo Katibu wa Shirika la VODIWATA Yuel Mnyonge, amesema wanashukuru kupewa msaada wa vifaa hivyo ikiwa vitakwenda kuleta mabadiliko makubwa kwenye utendaji wao wa kazi na jamii kwa ujumla, na kufahamu kuwa elimu jumuishi ndio mkombozi kwa watoto mwenye ulemavu.

Meneja wa mradi wa elimu jumuishi kutoka Shirika la Add International Adam Mkaka akizungumza kwenye kikao cha makabidhiano ya vifaa wezeshi(Laptop) kwa mashirikia ambayo yanajihusisha na watu wenye ulemavu.

Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Shinyanga Lidya Kwesigabo akizungumza kwenye kikao hicho cha makabidhiano ya vifaa wezeshi (Laptop) kwa mashirika ambayo yanajihusiha na watu wenye ulemavu.

Zoezi la utiaji saini likiendelea kwa ajili ya makabidhiano ya vifaa wezeshi (Laptop) kwa mashirika ambayo yanajihusisha na watu wenye ulemavu ili kuwaboreshea utendaji wao wa kazi katika kuwahudumia watu wenye ulemavu.

Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Shinyanga Lidya Kwesigabo, (wapili kulia) akimkabidhi Mmoja wa viongozi wa Taasisi ya Amani Kupyuta Mpakato (Laptop) kwa ajili ya kumrahisishia katika majukumu yake kuwa hudumia watu wenye ulemavu, (kulia) ni Meneja wa mradi wa elimu jumuishi kutoka Add International Adam Mkaka.

Zoezi la makabidhiano likiendelea la vifaa wezeshi (Laptop) kwa mashirika ambayo yanyojihusisha na watu wenye ulemavu.

Zoezi la makabidhiano likiendelea la vifaa wezeshi (Laptop) kwa mashirika ambayo yanyojihusisha na watu wenye ulemavu.

Washiriki wakiwa kwenye kikao cha makabidhiano ya vifaa wezeshi (Laptop) kwa mashirika ambayo yanajihusisha na watu wenye ulemavu.

Washiriki wakiwa kwenye kikao cha makabidhiano ya vifaa wezeshi (Laptop) kwa mashirika
 ambayo yanajihusisha na watu wenye ulemavu.

Washiriki wakiwa kwenye kikao cha makabidhiano ya vifaa wezeshi (Laptop) kwa mashirika ambayo yanajihusisha na watu wenye ulemavu.

Washiriki wakiwa kwenye kikao cha makabidhiano ya vifaa wezeshi (Laptop) kwa mashirika ambayo yanajihusisha na watu wenye ulemavu.

Washiriki wakiwa kwenye kikao cha makabidhiano ya vifaa wezeshi (Laptop) kwa mashirika ambayo yanajihusisha na watu wenye ulemavu.

Washiriki wakiwa kwenye kikao cha makabidhiano ya vifaa wezeshi (Laptop) kwa mashirika ambayo yanajihusisha na watu wenye ulemavu.

Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya kumalizika kwa zoezi la makabidhiano ya vifaa wezeshi (laptop) kwa mashirika ambayo yanajihusisha na watu wenye ulemavu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post