MAMA, MTOTO WAFARIKI KWA KUGONGWA GARI SHINYANGA MJINIWatu wawili ambao hawajafahamika mara moja, wamefariki dunia baada ya kugongwa na gari dogo linalotumika kwa shughuli binafsi ,wakati wakiwa wamemebwa kwenye Pikipiki maarufu kama bodaboda.

Tukio hilo limetokea leo mchana Oktoba 10,2022, kwenye eneo la karibu na shule ya msingi Kambarage, kata ya Kambarage katika Manispaa ya Shinyanga.

Mganga mfawidhi wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga Dkt. Luzila John, amesema watu hao ambao ni mama na mtoto wake kike anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya mwaka mmoja na miwili, wamefariki dunia kwa nyakati tofauti.

Dkt. Luzila ameeleza kuwa, Mama wa mtoto huyo amefikishwa hospitalini hapo akiwa tayari amefariki dunia, ambapo mtoto amefariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, kijana aliyekuwa akiendesha gari lililosababisha ajali hilo alikuwa amelewa.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Jackson Mwakagonda, amesema atatoa taarifa baadaye kuhusu tukio hilo.

Chanzo - Radio Faraja Fm

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post