CHAMA CHA WALIMU MANISPAA YA SHINYANGA CHAFANYA MKUTANO MKUU, SATURA AAHIDI KUSHUGHULIKIA MATATIZO YAO

Mwenyekiti wa chama cha walimu Manispaa ya Shinyanga Meshack Mashigala akizungumza kwenye mkutano huo.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

CHAMA cha Walimu Manispaa ya Shinyanga (CWT) kimefanya mkutano mkuu wa nusu mhula, huku wakimpongeza Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Jomaary Satura kwa kujali watumishi na kutatua matatizo yao.

Mkutano huo umefanyika leo Oktoba 21, 2022 katika ukumbi wa mikutano Shule ya Msingi Buhangija Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Mwenyekiti wa chama cha walimu Mkoa wa Shinyanga Mathias Balele , amesema Manispaa ya Shinyanga kwa sasa ina Mkurugenzi ambaye anajali maslahi ya watumishi wake, ambapo walimu wanapanda madaraja na kulipwa mapunjo ya mshahara, na katika halmashauri zote za mkoa huo Shinyanga ndiyo inaongoza kwa malipo hayo.

“Mkurugenzi tunakubali utendaji wako kazi, lakini tunakuomba tufikishie kilio chetu cha Teaching Allowance kirudi, ambacho kilikuwepo hapo awali lakini Serikali ilikiondoa, ili walimu wapate kipato cha ziada nje ya mshahara,”amesema Balele.

Naye Mwenyekiti wa chama cha walimu Manispaa ya Shinyanga Meshack Mashigala, amewasilisha baadhi ya changamoto ambazo zinawakabili walimu ikiwamo kupunguziwa nauli zao, pamoja na wengine kulipwa hadi watoke likizo, na kuomba walimu wanapaswa walipwe pesa zao kabla ya kwenda likizo.

Aidha, Katibu wa chama cha walimu Manispaa ya Shinyanga Allen Shuli, akisoma taarifa kwenye mkutano huo, amesema wamejikita kujadili mambo muhimu mawili ambayo ni kupokea taarifa ya utendaji kazi wa chama kwa kipindi cha miaka miwili na nusu tangu uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2020.

Pia kupokea na kujadili taarifa ya fedha mapato na matumzi kwa kipindi cha kuanzia Mei 2020 hadi Septemba mwaka huo.

Amesema sanjali na hayo pia wanamuomba Mkurugenzi kushughulikia tatizo la walimu waliopunjwa madaraja yao toka mwaka 2013 hadi 2022, jambo ambalo limesababisha walimu walioanza kazi pamoja kutofautiana mishahara, na hata walimu waliotangulia kazini kuzidiwa mishahara na wanafunzi.

Tatizo jingine ni mapunjo ya nauli na Posho ya kujikimu kwa walimu wapya ambao walilipwa kwa utaratibu wa zamani badala ya maelekezo mapya ya Serikali, mapunjo ya mishahara wanayodai walimu tangu mwaka (2013-2022) na fedha za uhamisho, nauli na matibabu.

Katika hatua nyingine, amesema wanasisitiza nidhamu, uwajibikaji na utii kwa walimu wote, pamoja na kukemea vitendo viovu vya kudhalilisha wanafunzi, ulevi, wizi wa mitihani pamoja na kukopa mikopo ya kupindukia.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura ambaye alikuwa mgeni Rasmi kwenye mkutano huo, amewasisitiza walimu suala la uwajibikaji na kuchapa kazi kwa bidii, wakati Serikali ikiendelea kushughulikia matatizo yao moja baada ya jingine.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura akizungumza kwenye mkutano mkuu wa chama cha walimu Manispaa ya Shinyanga.

Mwenyekiti wa chama cha walimu Mkoa wa Shinyanga Mathias Balele, akizungumza kwenye mkutano huo.

Mwenyekiti wa chama cha walimu Manispaa ya Shinyanga Meshack Mashigala akizungumza kwenye mkutano huo.

Katibu wa chama cha walimu Manispaa ya Shinyanga Allen Shuli, akisoma taarifa kwenye mkutano huo.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura akikata keki kwenye mkutano huo.

Mkutano Mkuu wa chama cha walimu Manispaa ya Shinyanga ukiendelea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

1/Post a Comment/Comments

Post a Comment