MAELFU YA WANANCHI SHINYANGA WAJITOKEZA KUPATA MATIBABU BURE YA MACHO, WAMPONGEZA MBUNGE LUCY MAYENGA KUWAJALI WANANCHI WAKE

 Wananchi wa Shinyanga wakiwa wamejitokea kwa wingi kupata matibabu bure ya macho kutoka kwa madaktari bingwa.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

WANANCHI wa Mkoa wa Shinyanga, wamejitokeza kwa wingi kupata huduma ya matibabu ya macho bure kutoka kwa madaktari bingwa, huku wakimpongeza Mbunge wa Vitimaalum mkoani Shinyanga Lucy Mayenga kwa kuratibu matibabu hayo.

Zoezi hilo la matibabu ya macho bure kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga limeanza kutolewa leo Oktoba 14, 2022 na litakwenda hadi Oktoba 16 siku ya jumapili, ambalo linafanyika katika Chuo cha Ualimu Shinyanga (SHYCOM) na limeratibiwa na Mbunge Lucy Mayenga.

Mayenga akizungumzia zoezi hilo, amesema ameguswa na wananchi wa Mkoa wa Shinyanga ambao walikuwa wakipata shida ya kupata huduma ya matibabu ya macho, kutokana na Mkoa huo kutokuwa na Madaktari bingwa wa macho wa kutosha, huku wengine wakishindwa kumudu gharama za matibabu.

“Mimi kama kiongozi Mwanamke nimeona nifuata nyayo za Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhudumia wananchi, ndiyo nikaona ni vyema ni ratibu zoezi hili la utoaji matibabu bure ya macho kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga,”amesema Mayenga.

“Matibabu haya yatachukua siku tatu na mimefurahi wananchi wamejitokeza wengi sana, na wale ambao watapelea kupata huduma hii, Madaktari hawa bingwa wa macho watarudi tena,”ameogeza.

Aidha, ametaja madaktari hao bingwa wa macho kuwa wanatoka katika Hospitali ya KCMC, AGHAKHAN, Mhimbili, Hindu na Madali ,huku akitoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga wajenge pia tabia ya kupima afya zao mara kwa mara, ili kupata matibabu mapema yakiwamo ya macho.

Naye Mratibu wa Taasisi ya Bilal Muslim Mission Of Tanzania Free eye Camp, ambaye pia ni kiongozi wa jopo la madaktari hao bingwa wa macho Ain Sharif, amesema katika zoezi hilo wanatarajia kutoa huduma ya matibabu ya macho kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga wapatao 3,500 hadi 4,000.

Nao baadhi ya wananchi wa Shinyanga ambao wamejitokea kupata huduma hiyo ya matibabu ya macho bure akiwamo Theonestina Rugambwa, wamemshukuru Mbunge Lucy Mayenga kwa kuwajali wananchi wake hasa wanyonge, na kumuomba aendelee na moyo huo huo wa kujali afya zao.

Mbunge wa Vitimaalum wa Mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga akizungumza kwenye zoezi la utoaji matibabu ya macho bure kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga.

Mratibu wa Taasisi ya Bilal Muslim Mission Of Tanzania Free eye Camp, ambaye pia ni kiongozi wa jopo la madaktari hao bingwa wa macho Ain Sharif, akizungumza namna wanavyotoa matibabu ya macho bure kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga.

Mratibu wa Taasisi ya Bilal Muslim Mission Of Tanzania Free eye Camp, ambaye pia ni kiongozi wa jopo la madaktari hao bingwa wa macho Ain Sharif, (kulia) akitetea jambo na Mbunge wa Vitimaalum Lucy Mayenga.

Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga (kulia) akitetea jambo wananchi katika zoezi hilo la utoaji matibabu ya macho bure.

Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga, akisaidia wananchi pamoja na watoto kwenda kupata matibabu ya macho bure kutoka kwa madaktari bingwa.

Wananchi wa Shinyanga wakiendelea kujitokeza kupata huduma ya matibabu ya macho.

Wananchi wa Shinyanga wakiwa wamejitokeza kupata huduma ya matibabu ya macho bure kutoka kwa madaktari bingwa.

Matibabu ya macho yakiendelea kwa wananchi wa Shinyanga kutoka kwa madaktari bingwa.

Matibabu ya macho yakiendelea kwa wananchi wa Shinyanga kutoka kwa madaktari bingwa.

Matibabu ya macho yakiendelea kutoka kwa madaktari bingwa.

Matibabu ya macho yakiendelea kutoka kwa madaktari bingwa.

Matibabu ya macho yakiendelea kutoka kwa madaktari bingwa.

Matibabu ya macho yakiendelea.

Wananchi wakipatiwa dawa za macho bure na wengine miwani mara baada ya kumaliza kupata vipimo.

Wananchi wakipatiwa dawa za macho bure na wengine miwani mara baada ya kumaliza kupata vipimo.

Matibabu ya macho yakiendelea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post