AUAWA KWA KUPIGWA RISASI BAADA YA KUVAMIA BENKI AKIJIHAMI KWA KISU


Polisi wamempiga risasi mwanaume aliyekuwa amejihami kwa kisu aliyejaribu kuiba katika Benki ya Equity tawi la Nairobi West mchana peupe.

Katika kisa hicho kilichofanyika Jumanne, Oktoba 11, mwanamume huyo alijaribu kunyakua pesa ambazo zilikuwa zikiwasilishwa benki humo na maafisa wa kampuni ya G4S.

Polisi walisema katika purukushani hizo, mtu anayeshukiwa kuwa jambazi aliwadunga visu watu watatu, maafisa wawili wa usalama na mteja wa benki, ambao walikimbizwa hospitalini. 

Mlinzi mmoja aliripotiwa kuwa katika hali mbaya.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Nairobi James Mugera alisema polisi waliokuwa wakisimamia benki hiyo walijibu kwa kumfyatula risasi jambazi huyo begani na tumboni.

Jambazi huyo pia alikimbizwa katika Hospitali ya Mabagathi, ambapo alikata roho.

Via Tuko News

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post