YANGA YATOKA SARE NA AZAM FC LIGI KUU YA NBC


MABINGWA watetezi Yanga wametoka nyuma na kutoka sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Matajiri wa Chamazi Complex Azam FC mchezo wa ligi Kuu ya NBC uliochezwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Shujaa wa Yanga ni Feisal Salum (Fei Toto) aliyetokea benchi na kwenda kufunga mabao yote mawaili dakika ya 56 na 77.

Azam FC walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa beki wao kisiki,Daniel Amoah dakika ya 24 akifunga bao kwa kichwa akimalizia faulo ya Ayubu Lyanga baada ya Yannic Bangala kumchezea rafu Prince Dube.

Hadi timu zinakwenda mapumziko Azam Fc walikuwa mbele ya bao hilo moja .

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko mnamo dakika ya 65 Malickou Ndoye aliifungia bao la pili Azam FC huku Yanga wakikosa Penalti iliyoadakwa na golikipa wa Azam FC iliyopigwa na Shaban Djuma baada ya Lusanjo Mwaikenda kumchezea rafu Benard Morrison.

Kwa Matokeo hayo Yanga wamefikisha mechi 40 wakicheza bila kufungwa na wanapanda mpaka nafasi ya kwanza wakiwa na Pointi 7 huku Azam Fc wakifikisha Pointi 5 Mechi nyingine imechezwa uwanja wa CCM Kiruma wenyeji Geita Gold wametoshana nguvu ya kufungana bao 1-1 na Kagera Sugar.

Ligi hiyo itaendelea kesho Simba watacheza na KMC katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments