MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO APEWA MAELEZO KUHUSU UTEKELEZAJI WA MFUKO WA KUENDELEZA UJUZI (SDF)


*******************

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Phillip Mpango leo tarehe 12 Septemba 2022 ametembelea banda la maonyesho la Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) na kupewa maelezo kuhusu utekelezaji wa Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) unaoratibiwa na TEA kwa ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Benki ya Dunia(WB).

TEA ni miongoni mwa za Taasisi zinazoshiriki maonyesho ya siku tatu ya Mkutano Mkuu wa 36 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania - ALAT yanayofanyika Jijini Mbeya kuanzia tarehe 12 Septemba, 2022.

Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Bahati Geuzye amesema mfuko wa SDF umetoa mafunzo kwa zaidi ya vijana elfu 37 kati ya vijana elfu 38 wanaolengwa kupatiwa mafunzo hayo hadi ifikapo Desemba 2022.

Akijibu swali la Makamu wa Rais kuhusu idadi ya vijana wanaotoka kaya maskini walionufaika na mafunzo ya kukuza ujuzi kupitia ufadhili wa SDF, Mkurugenzi Mkuu wa TEA alisema zaidi ya vijana 1,627 wamepata mafunzo hayo hadi sasa na kwamba vijana zaidi kutoka kundi hilo watapatiwa mafunzo ya kuongeza ujuzi kwa lengo la kuwezesha kupata ujuzi utakaowawezesha kujikwamua kiuchumi.

Makamu wa Rais alikuwa mgeni ramsi katika mkutano mkuu wa 36 Jumuiya za Tawala za Mitaa unaofanyika jijini Mbeya kwa siku tatu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post