KIPINI CHA PUANI KILICHOPOTEA MIAKA MITANO CHAKUTWA KWENYE MAPAFU

Joey Lykins (35)

JAMAA huyo wa nchini Marekani kwa jina la Joey Lykins (35) alilala alipoamka akawa hakioni kipini chake cha pua. Alihangaika kukitafuta kwa udi na uvumba bila mafanikio lakini miaka mitano baadaye kimekuja kuonekana katika mapafu yake.


Alianza kukohoa mfululizo huku akipata maumivu makali nyuma ya mgongo ilibidi akimbizwe hospitali ambapo awali daktari alidhani labda ni dalili za pneumonia lakini baada ya kupigwa x-ray picha ikaonesha ana kipini hicho cha pua ambapo alipooneshwa na daktari na kuulizwa kama anakumbukumbu zozote kuhusu kitu kama hicho akashangaa.


Ndipo akakumbuka miaka mitano iliyopita alipopoteza kipini chake baada ya kuamka akawa hakioni licha ya kukitafuta huku na huko.


Kwa bahati kipini hicho hakikupasua mapafu yake na ameweza kufanyiwa sajari kukiondoa ambapo sasa yupo vizuri ingawa hata yeye haamini ilikuwajekuwaje kikaingia mapafuni.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post