WAZIRI NAPE AIWAKILISHA TANZANIA UCHAGUZI WA KATIBU MKUU WA SHIRIKA LA MAWASILIANO DUNIANI - ITU

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Nape Moses Nnauye  ameiwakilisha Tanzania kwenye uchaguzi wa Katibu Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU) pamoja na Naibu wake, uliofanyika tarehe 29 Septemba, 2022 jijini Bucharest, Romania, kwenye Mkutano Mkuu wa ITU Plenipotentiary 2022 (ITU PP22).

Viongozi wanaochaguliwa kwenye Mkutano huo wataiongoza ITU kwa kipindi cha Miaka Minne kuanzia 2024 - 2027.

Waziri Nape mara baada ya uchaguzi huo, atatoa tamko la Kisera la Tanzania kwa wajumbe wa ITU PP22.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post