BINTI MDOGO ASHINDA NAFASI YA WAWAKILISHI WA WANAWAKE BUNGENI


Kutoka kijiji cha mbali cha Chemomul, kaunti ya Bomet, kutana na Linet chepkorir ‘Toto’, mwenye umri wa miaka 24 ambaye amepata kura 242,775 na kuwapiku wagombea wengine nane aliokuwa akishinda nao kwenye uchaguzi wa nchini Kenya.

Baadhi ya aliowapiku ni wanasiasa wenye uzoefu mkubwa.
Baba yake akimsaidia kunywa kinywaji cha kienyeji kinachojulikana kama ‘mursik’ kilichotengenezwa kwa maziwa ya siki na mkaa wa kitamaduni unaotumiwa kama ishara ya sherehe.


Linet chepkorir ‘Toto’, anakuwa Mwanamke mwenye umri mdogo zaidi kuwa mwakilishi Bungeni.

Hii ni kazi yake ya kwanza kabisa, Anatoka katika familia yenye uwezo wa hali chini, akiwa ni mtoto wa tatu kwa Bwana Richard langat na mkewe Bety langat.
Linet anasema ilikuwa ngumu kupambana dhidi ya washindani wenye mifuko mirefu, anakadiria kutumia kiasi cha shilingi ya kenya100,000 pekee kufanya kampeni na nyingine zilitoka kwa watu waliomtakia mema na marafiki wenye nia nzuri katika kisiasa.
Hii ni nyumba ya Linet, anatarajia kuboresha makazi yake na kufanya maisha ya wazazi wake kuwa bora zaidi. Hakuna huduma ya umeme katika kijiji chake

Ilikuwa ni shamrashamra, furaha, ngoma na machozi wakati kijiji kikimkaribisha nyumbani kwake, changamoto kubwa alipoanza mchakato wa kugombea ilikuwa ni kuishawishi jamii yake na wapiga kura kwa ujumla ambao walihoji kuwa hawezi kufanya hivyo kwa sababu hajaolewa, hana uzoefu wa kazi na hana pesa za kutoa.

Ujumbe wake kwa wasichana wote ‘usikate tamaa kamwe

CHANZO - BBC Swahili

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post