Na Alex Sonna
TIMU ya Taifa Stars imejiweka njia panda kufuzu Michuani ya Wachezaji wa ndani (CHAN) mashindano yatakayofanyika nchini Algeria 2023 baada ya kuchapwa bao 1-0 na Uganda mchezo uliopigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Akitokea benchi Mshambuliaji Travis Mutyaba aliwanyamazisha Watanzania waliohudhuria mechi hiyo dakika ya 87 baada ya kuchachafya ngome ya Taifa Stars.
Tanzania inahitaji kwenda kupindua meza mnamo tarehe 3 Septembar mwaka huu katika uwanja wa St.Mary nchini Uganda timu hizo zitarudiana
Mechi hiyo pia imehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi pamoja Balozi wa Marekani nchini Donald Wright.