******************************
Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo leo amewaongoza mamia ya wadau wa utamaduni, sanaa na michezo kuianza Siku ya Tamasha la Kuhamasisha Sensa la #Sensabika kwa mazoezi.
Tamasha hilo linaendelea mchana huu kwa muziki na ngoma na michezo mbalimbali na jioni kutakuwa na pambano la ngumi la bondia Karim Mandonga na kisha wasanii wakubwa chini watapanda stejini.
Mgeni rasmi katika Tamasha hilo atakuwa Mhe Mohammed Mchengerwa, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.