MAADHIMISHO SIKU YA NANENANE : MKE WA JAJI MKUU WA MAHAKAMA YA TANZANIA BI.MARINA JUMA AONGOZA WAKE WA MAJAJI KWENYE MATEMBEZI

Mke wa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Bi.Marina Juma (katikati) akiwaongoza wake wa majaji kwenye matembezi katika kuadhimisha siku ya Nanenane, matembezi ambayo yalianzia nyumbani kwake Jaji Mkuu wa mahakama ya Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma kupitia daraja la Tanzanite, Ocean Roads na kufikia tamati Serena Hotel.
*******************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

UMOJA wa wake wa majaji wa mahakama nchini (We are Family) wamejumuika pamoja katika kuadhimisha Siku ya Nanenane kwa kufanya matembezi ya umbali wa kilometa sita kupitia Tanzanite Bridge ambapo wake wa majaji 13 wameshiriki.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa matembezi hayo leo Jijini Dar es Salaam, mke wa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Bi.Marina Juma amesema wameamua kushiriki maadhimisho ya Nane nane wao kama kikundi wakaona ni muhimu kufanya matembezi ili kuimarisha afya zao.

Amesema matembezi hayo ni ya mara ya kwanza hivyo watahakikisha yanakuwa endelevu ambapo watakuwa wakikutana na kufanya mikutano ya mara kwa mara kujenga ushirikiano wa pamoja wao kama wake wa majaji nchini.

"Malengo hasa ya kikundi chetu ni kufanya mazoezi, kufahamiana na kuishi pamoja kama familia na kufanya mambo mbalimbali yenye manufaa na tija kwenye jamii". Amesema Bi.Marina Juma.

Pamoja na hayo amewakaribisha pia wake wengine wa majaji kuungana na kikundi hicho na kuweza kukutana mara kwa mara na kushiriki mazoezi kwa pamoja ili kuweza kuungana na kushirikiana kwa mambo mbalimbali.

Kwa upande wake mke wa Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania, Bi.Sada Othman ambaye amewawakirisha wake wa majaji wastaafu kwenye maadhimisho hayo amesema kuna umuhimu mkubwa hivyo amewataka wastaafu wengine wawe wanautaratibu wa kufanya mazoezi ili kuweka miili yao sawa kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza.

Baadhi ya wake wa Majaji wa Mahakama ya Tanzania wakiwa kwenye matembezi katika kuadhimisha siku ya Nanenane, matembezi ambayo yalianzia nyumbani kwake Jaji Mkuu wa mahakama ya Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma kupitia daraja la Tanzanite, Ocean Roads na kufikia tamati Serena Hotel. Mke wa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Bi.Marina Juma akiwaongoza wake wa majaji kwenye matembezi katika kuadhimisha siku ya Nanenane, matembezi ambayo yalianzia nyumbani kwake Jaji Mkuu wa mahakama ya Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma kupitia daraja la Tanzanite, Ocean Roads na kufikia tamati Serena Hotel. Wake wa Majaji wa mahakama ya Tanzania wakipata picha ya pamoja kwenye daraja la Tanzanite wakiwa kwenye matembezi katika kuadhimisha Siku ya Nane Nane ambapo wametembea kilomita sita. Wake wa Majaji wa mahakama ya Tanzania wakipata picha ya pamoja kabla ya kuanza matembezi katika kuadhimisha Siku ya Nane Nane ambapo wametembea kilomita sita wakipitia Tanzanite Bridge Jijini Dar es Salaam..

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments