KARANI WA SENSA ALIYEHESABU KAYA MOJA TU SIKU NZIMA NA KUKUTWA KALEWA AKAMATWA

 Mtu mmoja ambaye ni karani wa sensa mjini Musoma mkoani Mara, anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kutaka kujaribu kukwamisha zoezi la sensa kwa kuhesabu kaya moja tu kutwa nzima.


Mratibu wa Sensa wa Manispaa ya Musoma, Joseph Ochora amemtaja karani wa sensa, Thomas Ndyetabura kwamba anashikiliwa na polisi tangu juzi kwa kuhesabu kaya moja tu kutwa nzima na baadaye kukutwa akiwa amelewa.

Kwa mujibu wa Ochora, karani huyo alitakiwa kuhesabu kaya kati ya 20 hadi 30 kwenye Kata ya Kwangwa, lakini baada ya matendo hayo nafasi yake ikatolewa kwa karani mwingine na kazi inaendelea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post