AZAKI 89 ZAPEWA MAFUNZO YA USIMAMIZI RUZUKU KATIKA MPANGO KAZI WA MIAKA MITANO

Na Dotto Kwilasa, DODOMA


MKURUGENZI wa Shirika la Foundation For Civil Society (FCS) Francis Kiwanga amesema jumla ya Mashirika 86 kati ya 1200 yaliyoomba kupatiwa ruzuku, yamepewa ruzuku ya shilingi Bilioni.4 ili kutekeleza miradi ya maendeleo chini ya program ya utawala bora katika sekta za maji,elimu afya na kilimo.


Akizungumza leo Jijini Dodoma wakati wa mafunzo ya usimamizi wa ruzuku katika Mpango kazi mpya wa miaka mitano, Mkurugenzi huyo amesema FCS imejikita katika kuhakikisha miradi inayofadhiliwa inawasaidia wananchi katika kuboresha maisha yao na kukuza sekta ya asasi za kiraia.


"Tumeanza msimu mpya, niwasihi sana kutumia fursa hii vizuri bila udanganyifu,tutakuwa wakali kweli kweli lengo letu hizo fedha lazima ziende sehemi inavyotakiwa,lazima Asasi zote zitambue kuwa wao ndio wanatusaidia kutatua kero za wananchi, sisi ni wacheche hatuwezi kuifikia nchi nzima,"amesema Mkurugenzi huyo.


Amesema kuwa taasisi zilizoomba zilikuwa zaidi ya 1200 kutoka Tanzania nzima lakini taasisi zilizofanikiwa 86 hivyo hizo fedha zimegawanywa kwenye mikoa yote na wadau wote ambao wanafanya kazi nao kwa mwaka huu.


Kiwanga amesema FCS imetoa ruzuku kiasi cha bil.4 kwa mwaka huu na wadau wote watafanya kazi kwa mwaka huu na mwakani,hivyo wameweza kupata wadau 86 wanaotoka katika mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani, ambao watakuwa wanafanya kazi kusukuma agenda ya utawala bora nchini.


Ametaja maeneo ambayo watayafanyia kazi kuwa ni pamoja na Afya elimu,ulinzi na amani na kueleza kuwa kumekuwa na ushindani wa kisiasa na kwa sababu ya ushindani huo migogoro haikosekani hivyo ni lazima pia kushughulikia eneo hilo ili amani iendelee kuwepo.


"Eneo lingine ni ardhi ,bado usawa katika umiliki wa ardhi haupo hivyo kupitia AZAKI hizi kazi yao ni kusukuma ajenda ya usawa wa kijinsia, maji na kilimo,tuna Imani kuwa Mkataba tuliofanya leo utaenda kuongeza utendaji Kazi na uwajibikaji,"amesema


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Tanzania Women for Initiative lenye makazi yake mkoani Tanga Benadeta Choma amesema kuwa Ruzuku zinazotolewa na serikali na wafadhili zinawasaidia kujenga uelewa wa wananchi na hasa katika sekta ya afya .


Amesema kupitia ruzuku hiyo wataenda kuboresha afya ya jamii katika Wilaya ya Nkinga kwa kuona yale ambayo mpango mkakati wa wilaya hiyo kuhusu wapi wamefikia na wapi wamekwama na nini kifanyike ikiwa ni pamoja na kufanya ufuatiliaji wa karibu.


"Kama meneja wa mradi matarajio yangu ni kuona matokeo yaliyotarajiwa kwa Wananchi yanafanikiwa ikiwemo miradi yote inayohusu ulemavi ,Jinsia na usimamizi wa rasilimali,"amesema

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post