MENEJA SHIRIKA LA RELI 'TRC' AKIRI KUFUKUZWA KAZI AKIPINGA TOZO


Aliyekuwa Meneja wa Shirika la Reli, Kanda ya Dar Es Salaam, Jonas Afumwisye.

 **
SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) limemfukuza kazi meneja wake wa kanda ya Dar es Salaam, Jonas Afumwisye kwa kuzipinga  tozo za miamala kwenye makundi ya kijamii.


Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa alimwandikia barua Afumwisye kumjulisha kuhusu uamuzi huo Agosti 19, 2022 baada ya kuthibitika kwa tuhuma zilizokuwa zikimkabili.


Afumwisye amekiri kupokea barua hiyo juzi Agosti 22, ila akasema anakusudia kukata rufaa Tume ya Utumishi wa Umma kama sheria inavyoelekeza.“Ni kweli nimepata hayo matatizo…utaratibu unaofuata ni kukata rufaa ndani ya siku 45, ” alisema Afumwisye alipoulizwa.Baada ya meneja huyo kuthibitisha kupokea barua ya kufutwa kazi, Rais wa Chama cha Wafanyakazi nchini amesema wanapinga hatua hiyo kwa kuwa alitimiza haki yake ya kutoa maoni.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post