HIZI NDIYO SIFA NA UZURI WA WATU WENYE MACHO MAKUBWA


KATIKA uumbaji wa mungu aliumba binadamu wenye sifa mbalimbali. Je ulishawahi kujua watu wenye macho makubwa wana sifa zipi Zaidi ya zile kama upole na vinginevyo. 

Zijue zaidi sifa zao nyingine ambazo utakua likua hujui kabisa au ulikuwa tu na nadharia kuhusu watu wenye macho makubwa.

1.Wana roho nzuri zaidi

Ikiwa ni kweli kwamba unaweza kujua nafsi ya mtu kwa kumuangalia machoni pake basi Mungu alikuwa na awapendao zaidi wakati wa uumbaji wa binadamu. Inasemekana ukubwa wa macho unaendana na uzuri wa roho ya mtu.Unaweza kusema kwamba mioyo yao ni safi na hawatataka kamwe kukuumiza. Taswira ya macho yao hufunua sehemu zao za ndani kabisa na kukuonyesha kuwa unaweza kuwashirikisha zaidi mambo, haijalishi ni nini.


2.Ni marafiki wa kweli na wanajali

Sura zao huvutia watu wengi kujenga urafiki nao na kuwashirikisha mambo mengi, katika hilo macho yao huonyesha ukweli wa mioyo yao yenye upole na kujali.Hali hiyo huwafanya watu kujenga ukaribu nao zaidi ya watu wengin, na kadiri unavyojenga nao ukaribu ndo unazidi kutambua kua mawazo yako ya kwamba wana roho nzuri ni ya kweli. Na hupenda zaidi kuwafanya watu wao wa karibu kua na furaha muda wote hawapendi kuona mwingine akiumia.


3.Ni watu wanaojitolea sana

Ulishawahi kumuangalia mtu mwenye macho makumbwa akiwa anafanya kazi zake, huwa wnaweka akili yote kwenye kazi ili kutoa kilicho bora zaidi.Hata kwenye mahusiano yao huwa ni watu wanapenda kweli hawapendi kusaliti wakipenda wanatoa mioyo yao kwa watu waliowapenda. Hujitoa katika kila hali kuonyesha kua hawatakata tamaa juu yako.


4.Ni watu wenye ushawishi zaidi

Kutokana na kua kila kitu huwa kinajionesha kwenye macho, huwa na urahisi wa kufanya mtu akubaliane nae hata kama palikua na ugumu kwenye jambo fulani. Hujitahidi kuelezea hisia zao kupitia macho na pale mnapotazamana tu utaweza kugundua nini wanakimaanisha.


5.Ni watu wasiokata tamaa kiurahisi

Watu wenye macho makubwa wana ujasiri. Wanajua jinsi ya kujitetea wenyewe na ni vigumu kuacha malengo na imani zao.Ukiwapa kazi, watafanya lolote wawezalo ili kuikamilisha kazi hiyo. Na hata ikitokea wameshindwa watatafuta suluhisho la kukamilisha kazi hiyo kwa namna yoyote bila kukata tamaa.


Imeandikwa: Dunstan Mtili Erick kwa msaada wa mitandao

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post