Mamlaka nchini Somalia zinasema kuwa takribani watu 10 wameuawa baada ya kundi la al-Shabab kuvamia hoteli moja iliyopo katika mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu.
Polisi wamesema kuwa washambuliaji hao walitega mabomu mawili nje ya hoteli hiyo kabla ya kuingia ndani na kuanza kufyatua risasi.
Kikosi maalum cha polisi kimesema kuwa kilifanikiwa kuwaokoa makumi ya wageni na wafanyakazi waliokua kwenye hoteli hiyo ya Hayat.
Mmoja wa maafisa hao aitwae Mohamed Abdikadir amesema kuwa "Vikosi vya usalama vimeendelea kupambana na vikosi hivi vya kigaidi , tumefanikiwa kuokoa watu wengi ila tuna taarifa za raia wa8 kupoteza maisha mpaka sasa".
Tovuti moja inayohusiana na Al-Shabab ilithibitisha kundi hilo kufanya uhalifu huo