Rais Mteule wa Kenya William Ruto na Mwanasiasa Mkongwe Raila Odinga
**
BAADA ya matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Kenya Rais Mteule William Ruto Ameongea na waandishi wa habari na kusema watashiriki katika wito wowote utakaotolewa na Mahakama juu ya matokeo ya uchaguzi.
Mpinzani wa Rais huyo mteule ambaye pia ni mwanasiasa mkongwe wa Kenya Raila Odinga alipinga matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo.
Katika kufuata demokrasia Odinga alisema atafungua kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu huo uliofanyika Agosti 9.
Rais Mteule wa Kenya William Samoei Ruto
Ruto amezungumza na waandishi wa habari baada ya kukutana na viongozi waliochaguliwa kutoka muungano wake wa kisiasa. Ruto amesema matarajio ya Wakenya ni makubwa na anaendelea na juhudi za kuunda serikali yake, ambayo haitamtamfungia nje yeyote kwa misingi ya chama au kabila.
Imeandikwa: Dunstan Mtili Erick kwa msaada wa mitandao