OJADACT YAWANOA WAANDISHI WA HABARI KANDA YA ZIWA KUANDIKA HABARI MWENDELEZO ZA SENSA

 Mwenyekiti wa OJADACT bwana Edwin Soko akizungumza wakati mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu kuandika habari za sensa kwa mwendelezo, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi. 


Na Mwandishi wetu Mwanza

Chama cha waandishi wa habari wa kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu Tanzania(OJADACT) kimeendesha mafunzo kwa kundi la waandishi wa habari ili kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuandika habari za sensa kwa mwendelezo.

Mgeni Rasmi kwenye mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi ameipongeza OJADACT kwa ubunifu huo wa kuandaa mafunzo ya kuwafanya waandishi wa habari kuwa na tabia ya kuendeleza habari za sensa hata kama sensa itapita.

"Huu ni ubunifu wenye faida kubwa kwa Taifa kwa kuwa kuendelea kuandika habari za sensa itaisadia jamii kujenga uelewa wa umuhimu wa kushiriki zoezi la sensa Nchini, hivyo niwapongeze waandishi wa habari kujifunza zaidi kwenye mafunzo haya ya leo", amesema Makilagi.

Pia  amesema kuwa, sensa ina faida kubwa sana kwa Taifa katika nyanja zote za uchumi, jamii na kisiasa, kwani bila kuwa na idadi kamili ya watu wako ni ngumu kutekeleza maendeleo.

Mwenyekiti wa OJADACT bwana Edwin Soko amewahamasisha waandishi wa habari waendelee kuandika habari mwendelezo za sensa kwani hii itasaidia kujua umuhimu wa sensa kwa Taifa na wajibu wa serikali kwenye kuleta maendeleo.

Soko pia amewataka waandishi pia kufuata maadili ya uandishi wa habari pindi wanapoandika habari mwendelezo za sensa.

Soko amewashukuru Taasisi ya MYCN,  Furaha Nyanza Co.LTD , Toto Gift Shop na Desk and Chair Foundation kwa kufanikisha mafunzo hayo ya kuandika habari za sensa yaliyoandaliwa na OJADACT.

Mratibu wa OJADACT Lucyphine Kilanga amewakumbusha waandishi wa habari kwenye kujua historia za sensa kuanzia sensa ya kwanza ya mwaka 1910 na hadi sensa ya tano ya mwaka 2002 na kubainisha wajibu wa kila mtanzania kushiriki kwenye sensa.

Kwa upande wake mshiriki Alphonce  Tonny toka Mkoa wa Mwanza amesema kuwa mafunzo hayo yamempa mtazamo mpya kwa waandishi wa habari kwani mwanzoni walijua wajibu wao ni kuandika tu habari za sensa na ikipita basi kazi imeisha lakini kumbe bado kuna umuhimu mkubwa wa kufanya mwendelezo wa habari za sensa ili jamii ielewe umuhimu wa sensa .

Naye mshiriki Mwamvita Issa toka Mkoa wa Shinyanga amesema kuwa, mafunzo hayo yamemjengea uwezo mkubwa wa kujua namna bora ya kuendelea kuandika habari za sensa.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi akizungumza wakati mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu kuandika habari za sensa kwa mwendelezo
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi akizungumza wakati mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu kuandika habari za sensa kwa mwendelezo
Mwenyekiti wa OJADACT bwana Edwin Soko akizungumza wakati mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu kuandika habari za sensa kwa mwendelezo
Mwenyekiti wa OJADACT bwana Edwin Soko akizungumza wakati mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu kuandika habari za sensa kwa mwendelezo
Mratibu wa OJADACT Lucyphine Kilanga akizungumza wakati mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu kuandika habari za sensa kwa mwendelezo
Mshiriki Alphonce  Tonny toka Mkoa wa Mwanza akizungumza wakati mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu kuandika habari za sensa kwa mwendelezo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments