DK. KALEMANI: TUJITOKEZE KUHESABIWA KWA AJILI YA MAENDELEO


MBUNGE wa Jimbo la Chato,Dk. Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa Chato

Na Daniel Limbe,Chato

MBUNGE wa Jimbo la Chato,Dk. Medard Kalemani amewataka wananchi kushiriki kikamilifu kwenye zoezi la sensa ya watu na makazi Agosti 23,2022.

Kauli hiyo ameitoa leo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya zamani vya stendi ya zamani ya Chato wakati akiwahamasisha wananchi kuhesabiwa.

Aidha amedai kufahamika kwa idadi ya watu na makazi yao itasaidia serikali kupanga maendeleo toshelevu kwa jamii.

"Ninawahamasisha ndugu zangu tujitokeze kuhesabiwa kwa ajili ya maendeleo...tunataka kuonyesha kuwa Chato tuko wengi ", amesema Dk. Kalemani.

Kadhalika amewataka kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali kusogeza maendeleo kwa wananchi hali itakayosaidia wananchi kujiletea maendeleo kwa wakati.

"Jambo la kwanza niwaombe sana mjitokeza kuhesabiwa...pili kuunga mkono juhudi za serikali...tatu kushikamana na mwisho ni kuchapa kazi kwa bidii"amesema.

Hata hivyo amewahakikishia wananchi wa wilaya ya Chato kuwa serikali inaendelea kutoa fedha nyingi za maendeleo ya wilaya hiyo ili kuhakikisha malengo yaliyokusudiwa yanatimia.

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Chato, Mandia Kihiyo,amesema kuwa taratibu zote za maandalizi ya zoezi la sensa zimekamilika na kwamba wananchi wanapaswa kutoa ushirikiano mkubwa kwa makalani wote wakataopita kwenye makazi Yao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments