AFARIKI KWA KUTUMBUKIA KWENYE SUFURIA YA UJI



Picha za CCTV zimeonesha rejeo la tukio

MWANAUME mmoja nchini India aliyefahamika kwa jina la Muthukumar amefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye sufuria kubwa lililokuwa limejaa uji wa moto uliokuwa ukiendelea kuchemka jikoni.


Muthukumar alionekana akiwa mmoja wa wapishi wanaolinda masufuria hayo tayari kwa uji huo kunywewa katika tamasha huko Tamil Nadu Madurai nchini India, Julai 29, 2022.



Video ya CCTV iliyorekodi tukio zima, imeonyesha kusambaa ikimuonesha jamaa huyo akiwa amekaa ndani ya sufuria na watu wakimkimbilia kwenda kumuokoa.


Muthukumar alipelekwa hospitali ya Rajaji akiwa na majeruhi asilimia 65 ya mwili wake hali iliyosababisha kifo chake Jumanne, Agosti 2, 2022.


Tamasha la ‘Aadi Velli’ ni tamasha kubwa na muhimu kwa jamii ya Tamil Nadu ambapo uji hupikwa na kugawiwa kwa watu wanaoheshimika wakipewa jina la Goddess Amman.


Haijajulikana mara moja ni nini kilimfanya atumbukie kwenye sufuria hilo, lakini mke wake anasema mume wake alikuwa na kifafa na huenda ndicho kilichosababisha akaangukia kwenye uji huo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post