RUTO AFUNGUKA KWA MARA YA KWANZA BAADA YA UCHAGUZI MATOKEO YA URAIS KENYA YAKISUBIRIWA


Kwa mara ya kwanza tangu uchaguzi mkuu nchini Kenya, mgombea urais William Ruto amehutubia umma siku ya Jumapili.

Ruto aliwashukuru Wakenya kwa kupiga kura katika uchaguzi huo wakati wa ibada ya kanisa nyumbani kwake Karen iliyohudhuriwa na washirika wake wa kisiasa.

"Nataka niwashukuru Wakenya wote, milioni kumi na nne waliojitokeza kupiga kura ndio tuwe na kiongozi mwingine wa miaka ijayo," alisema Ruto.

Kulingana na kiongozi huyo, baada ya Wakenya kupiga kura kumchagua rais wao ajaye, Mungu ndiye mwenye uamuzi wa mwisho kuhusu nani atakuwa kiongozi ajaye wa nchi.

Ruto pia aliendelea kuwapongeza viongozi kutoka vyama mbalimbali walionyakua viti mbalimbali katika uchaguzi uliokamilika.

“Tunawapongeza viongozi wote walioshinda hata tunaposubiri kwa amani hatua inayofuata, ili kukamilika kwa mchakato wa uchaguzi,” aliongeza.

Wakati huo huo, Ruto aliwataka Wakenya kuwa na subira na IEBC huku shughuli ya kuthibitishwa katika Bomas of Kenya ikiendelea.

Via >> BBC Swahili

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post