KAULI YA ODINGA WAKENYA WAKISUBIRI MATOKEO YA URAIS KUTOKA KWA IEBC

Mgombea wa Urais wa Muungano wa Kenya Raila Odinga amewataka Wakenya kudumisha amani hata wanaposubiri matokeo ya urais kutoka kwa IEBC.

Raila alimshukuru Mungu kwa amani ambayo imetanda nchini tangu Jumanne, Agosti 9,2022 Wakenya walipoenda kupiga kura kuwachagua viongozi wapya.

Akizungumza katika Kanisa la ACK St. Francis huko Karen, alikohudhuria ibada ya Jumapili, Raila alisema haikuwa rahisi kwa Azimio kupitia kipindi cha uchaguzi, lakini wanamshukuru Mungu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post