BENKI YA NBC YAKABIDHI MATREKTA YA MIKOPO KWA WAKULIMA


Wakulima wakiwa na Matrekta ya Mikopo ambayo wamekopeshwa na Benki ya NBC.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) Tawi la Shinyanga, imekabidhi Matrekta Mawili ya Mikopo kwa Wakulima ili kuunga juhudi za Serikali kukuza Sekta ya Kilimo na uchumi wa Taifa.

Matreka hayo yamekabidhiwa leo Agosti 13 ,2022 na Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, hafla iliyo hudhuliwa pia na Kampuni ya usambazaji wa zana za Kilimo Agricom.

Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Shinyanga Joyce Chagonja, akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi Matreka kwa wakulima, amesema Benki hiyo ina fursa nyingi za mikopo kwa ajili ya wakulima ikiwamo kuwakopesha zana za kilimo, pamoja na Bima za mazao.

Amesema ukopeshaji wa Matrekta hayo hakuna masharti magumu, bali ni Mkulima anatakiwa awe na Shamba, pamoja na kuchangia asilimia 25 ya Mkopo wake, huku wao wakichangia asilimia 75 na Marejesho yake ni nafuu hayambani Mkulima.

“Matrekta ambayo tumekabidhi wakulima hawa leo gharama zake ni Sh. milioni 40.7 kwa kila Moja na wakulima hawa wamechangia asilimia 25,”amesema Chagonja.

“Benki ya NBC tupo pamoja na Serikali kukuza Sekta ya Kilimo sababu tunatambua kuwa kilimo ndiyo uti wa mgongo asilimia 80, na ndiyo maana leo tumekabidhi Zana hizi za kilimo kwa wakulima,”ameongeza.

Naye wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, ameipongeza Benki hiyo ya NBC kwa kuunga mkono juhudi za Serikali kukuza Sekta ya kilimo na kutoa mikopo Zana za kilimo kwa wakulima, huku akitoa wito kwa wakulima kuzitumia zana hizo kufanya kilimo chenye tija na kuongeza kasi ya uzalishaji wa mazao.

Nao baadhi ya wakulima walionufaika na mikopo hiyo ya Matrekta akiwamo Golea Kamata na Bujiku Fumbuka, amesema Zana hizo za kilimo zitakwenda kuwa chachu ya mabadiliko na kukuza uchumi wao na taifa kwa ujumla kupitia Sekta hiyo ya Kilimo.

Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Shinyanga Joyce Chagonja, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Matrekta kwa wakulima.

Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi Matrekta kwa wakulima

Meneja wa Kampuni ya Agricom Kanda ya Ziwa Christina Mabula, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi Matrekta kwa wakulima.

Muonekano wa Matrekta ya Mikopo kwa wakulima.

Wakulima wakiwa na Matrekta ya Mikopo ambayo wamekopeshwa na Benki ya NBC.

Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko (kulia) akikabidhi funguo kwa Mkulima Golea Kamata ambaye amekopeshwa Trekta na Benki ya NBC.

Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko (kushoto) akikabidhi funguo kwa Mkulima Bujiku Fumbuka ambaye amekopeshwa Trekta na Benki ya NBC.

Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya wakulima kumaliza kukabidhiwa Matrekta ya mikopo na Benki ya NBC.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post