BABU WA MIAKA 74 AFANYA HARUSI YA KUKATA NA SHOKA AKIOA KWA MARA YA KWANZA KABISA



Mwanamume mwenye umri wa miaka 74, anagonga vichwa vya habari kwa kuoa mara ya kwanza katika maisha yake.


Mallam Muhammad Awal, 74, alifanya harusi ya kukata na shoka na barafu wake wa moyo mwenye umri wa miaka 45, Mallama Rahmat. 

Mallam Muhammad Awal, kutoka jimbo la Kogi, Nigeria, alifanya harusi ya kukata na shoka na barafu wake wa moyo mwenye umri wa miaka 45, Mallama Rahmat Muhammad mnamo Jumapili, Agosti 28,2022.


Akizungumza na wanahabari, mkongwe huyo alisema alisubiri muda mrefu kabla ya kuoa kwa sababu ya ukosefu wa rasilimali na fedha.


Anasema changamoto hizo zilimkatisha tamaa ya kumkaribia mwanamke na kumposa akihofia kuwa huenda angemhadaa na mwanaume mwingine.


"Siku zote nimekuwa nikiogopa kwamba ninaweza kushindwa katika jukumu langu la kumtunza mwenzi wangu ikiwa nitaoa na ni jambo ambalo ninaogopa na sitaki kutania. Pia ninaogopa kutengana na mwenzi wangu."


"Najua nikishindwa kumtunza anaweza kuniacha au kunilaghai na mwanaume mwingine jambo ambalo nisingependa. Kwa hiyo, ili kuepuka hayo yote, nilitupilia mbali wazo la ndoa kabisa. Lakini sasa, Mwenyezi Mungu amefanya jambo hili kuwa kweli. Wengi wao walinidharau, hasa kwa sababu ya hali yangu ya kifedha. Lakini namshukuru Mungu ni huko nyuma," alisema.


Akizungumzia kilichomvutia kwa mkewe na iwapo ana mpango wa kuzaa naye, alisema:


“Mbali ya kuwa ni mrembo, pia ni mtu wa chini kwa chini, muelewa, wa kidini na amejikita katika taasisi ya ndoa. Ni Mwenyezi Mungu pekee ndiye anayejua kama tutapata watoto. Huwezi kujua kile ambacho Mwenyezi anaweza kufanya. Haiko mikononi mwetu, bali mikononi Mwake.”


Kwa upande wake, bibi harusi Rahmat alisema kwamba ilikuwa imepangwa na Maulana kuwa watakuwa wanandoa.


Chanzo: TUKO.co.ke

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments