WAZIRI MKUU WA UINGEREZA AJIUZULU..ASEMA 'NI UPUUZI KUBADILISHA SERIKALI"

 

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amejiuzulu wadhifa wake. Akitoa hotuba yake:

Johnson: Nina huzuni kuacha kazi bora zaidi duniani,

‘’Ninataka ujue jinsi ninavyohuzunishwa na kuacha kazi bora zaidi duniani,’’ waziri mkuu anasema.

"Nimekubaliana na Sir Graham Brady, mwenyekiti wa wabunge wetu wa viti maalum, kwamba mchakato wa kumchagua kiongozi mpya uanze sasa na ratiba itatangazwa wiki ijayo. Na leo nimeteua Baraza la Mawaziri kuhudumu, pia nitaendelea kuongoza hadi kiongozi mpya atakapochaguliwa.’’

''Inatia uchungu kutoona miradi yangu ikikamilika''

Johnson anasema ni upuuzi kubadilisha serikali – na kukataa wazo la uchaguzi mkuu - wakati ‘’tunatimiza majukumu mengi na makubwa hali ya kiuchumi ikiwa ngumu sana ndani na kimataifa’’.

‘’Najuta kutofanikiwa katika majadiliano na inatia uchungu kutoona mawazo na miradi mingi ikitimia.’’


Via BBC Swahili

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments