POLISI YATANGAZA KIAMA KWA WALIOFANYA MAUAJI KIGOMA


Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Liberatus Sabas akizungumza na wananchi kwenye kijiji cha Kiganza wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma kulipotokea mauaji ya watu sita juzi.(Picha na Fadhili Abdallah)

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

JESHI la polisi nchini limetangaza kuunda kikosi maalum kitakachofanya uchunguzi wa tukio la kuuawa kwa watu sita wa familia moja katika kijiji cha Kiganza halmashauri ya wilaya Kigoma mkoani kigoma usiku wa kuamkia Jumapili.

Kamishna wa operesheni na mafunzo wa jeshi la polisi nchini,kamishna wa Polisi Liberatus Sabas alisema hayo akizungumza na waandishi wa habari eneo la tukio ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Mkuu wa jeshi la polisi nchini (IGP)Simon Sirro.

Sabas alisema kuwa hakuna atakayepona ambaye amehusika na tukio hilo na kwamba polisi wakisaidiana na vikosi vingine vya ulinzi na usalama wameanza kazi kuhakikisha wahalifu wote waliohusika na tukio hilo wanakamatwa haraka iwezekanavyo.

Kamishna huyo wa Operesheji na mafunzo wa jeshi la polisi alisema kuwa tayari timu ya wataalam wa uchunguzi imeshaanza na timu nyingine ya uchunguzi ya jeshi la polisi kutoka makao makuu ya polisi Dododma ipo njiani kwa ajili ya kuja kushiriki kwenye zoezi la uchunguzi na upelelezi kuwatafuta wahalifu waliohusika na tukio hilo.

“Hakuna mtu yeyote aliyehusika anayeweza kukwepa mkono wa dola hivyo tumejipanga kuhakikisha watu hao wanakamatwa,tunaowamba wananchi wa eneo hilo kutoa taarifa ambazo zitalisaidia jeshi la katika kufaniki upelelezi wake,”Alisema Kamishna Sabas

Pamoja na yote Kamishana huyo wa operesheni na mafunzo amewaonya watu wenye taarifa kuhusiana na tukio hilo kutoa taarifa hizo sasa lakini wakaficha au kuwa ni sehemu ya tukio hilo wakibainika watashughulikiwa ipasavyo.

“Lazima jibu lipatikane ndani ya muda mfupi, kuna watu wameingiwa na pepo la kukosa hofu ya Mungu na kuwauwa wenzao kama kuku, Naomba wote wenye taarifa au kufahamu chochote kuhusiana na tukio hilo watoe taarifa na taarifa hizi zitakuwa za siri na watoa taarifa wote watalindwa ukiacha na tukajua itakuwa tatizo kubwa kwako,”alisema Mkuu huyo wa Operesheni na Mafunzo

Katika hatua nyingine mtoto James Januari (4) aliyelazwa Hospitali ya mkoa Kigoma Maweni baada ya kujeruhiwa vibaya kwenye tukio hilo anaendelea na matibabu hospitalini hapo.Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo,Dk. Stanley Binagi amesema kuwa mtoto

kwa sasa mtoto huyo amelazwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) kwa ajili ya uangalizi zaidi.Dk.Binagi alisema kuwa mpango uliopo kwa sasa ni kumpa rufaa mtoto huyo kwenda hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.Jumla ya watu sita wa wa familia moja akiwemo bibi kizee mwenye umri wa miaka 70 aliyefahamika kwa jina la Tilifera Toyi (70) wameuawa kwa kukatwa katwa na vitu vyenye ncha kali kichwani na kwenye maeneo mbalimbali ya miili yao na watu ambao hawajafahamika hadi sasa.

Hadi leo hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusiana na tuhuma za mauaji hayo ambapo miili ya marehemu wote sita ilizikwa kijijini Kiganza juzi jioni (Jumapili)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments